Je,Wajua Mdomoni Kuna zaidi ya aina 700 za bakteria zinazojulikana?
Fahamu Mdomoni,Kuna zaidi ya aina 700 za bakteria zinazojulikana, pamoja na vimelea vingine kama vile, virusi na protozoa.
Viumbe hivi vyote vinaweza kuonekana tu kwenye maabara, na vina jukumu muhimu katika kulinda afya yako.
Magonjwa ya kawaida yanayosababishwa na bakteria hawa ni kuoza meno na ugonjwa wa fizi.
Baadhi ya Tafiti Zinaonyesha viumbe hivi pia vinahusika na hali nyingine mbaya za afya zinazotokea katika mwili wa binadamu.
Yapo baadhi ya Magonjwa ambayo hutokana na shida hii ya Mdomo,Ikiwemo;
✓ Ugonjwa wa mapafu
Kwa kuwa kuvuta pumzi huanzia mdomoni na kisha kwenye mapafu, haishangazi kwamba baadhi ya viumbe vilivyo kinywani huishia kwenye mapafu.
Na mara nyingi husababisha magonjwa kama vile nimonia, Maambukizi haya hutokana na kutokufanya usafi wa mdomo na kusababisha bakteria kukua.
Kulingana na utafiti, usafi wa kinywa unaweza kupunguza bakteria hawa.
✓ Ugonjwa wa moyo
Moja ya magonjwa yanayosababishwa na viumbe wa mdomoni ni kuoza meno.
Ugonjwa huo ni uvimbe unaosababisha uharibifu wa mfupa wa jino pamoja na mizizi midogo ndani yake, na hatimaye husababisha jino kung’olewa.
Ugonjwa huu husababishwa na bakteria kukua kati ya ufizi na meno, kutokana na kutokufanya Usafi vizuri wa kinywa.
Lakini jambo ambalo limewashangaza watafiti kwa miaka mingi ni uhusiano kati ya ugonjwa wa fizi na ugonjwa wa moyo.
Uhusiano huu unaweza kuwa ni kutokana na mambo kadhaa. Mfano, watu wanaovuta sigara au kemikali za sumu – huwa na ugonjwa wa fizi na ugonjwa wa moyo.
Watafiti wengine pia wameripoti kwamba bakteria katika mifupa ya pua wanaweza pia kusafiri kwenda kwenye moyo, na kusababisha maambukizi. Ingawa hilo bado halina ushahidi wa kutosha.
✓ Matatizo ya kumbukumbu
Moja ya magonjwa ya kushangaza zaidi yanayohusiana na usafi wa mdomo ni kupoteza kumbukumbu.
Madaktari wa kinywa huhusisha usafi wa kinywa na matatizo ambayo husababisha kupoteza kumbukumbu au kuchanganyikiwa.
Mara nyingi matatizo ya kumbukumbu na matatizo ya meno hutokea uzeeni, ni vigumu kuamua ikiwa kuna uhusiano kati ya magonjwa mawili.
Lakini mwaka 2019, kikundi cha watafiti kiliripoti, ubongo wa watu wenye shida ya akili una bakteria wa P gingivalis, ambao ni moja ya bakteria wakuu wanaosababisha ugonjwa wa fizi.
Ingawa wazo kwamba ubongo, ambao ni sehemu safi zaidi katika mwili wa binadamu, huathiriwa na bakteria kutoka kinywani bado linahitaji utafiti zaidi. Halijakubalika na wataalamu wengi.
Pia, ugonjwa wa moyo na kupoteza kumbukumbu kuhusishwa na bakteria kutoka mdomoni, yanahitaji utafiti zaidi.
Ijapokuwa athari za uchafu wa kinywa zinaonekana kuongezeka, habari njema ni kwamba tuna uwezo wa kudhibiti uchafu na kuishi vyema na bakteria waliopo katika vinywa vyetu, na tunaweza kuzuia magonjwa.
Kudumisha usafi wa mdomo ni muhimu. Miongoni mwa mambo unayoweza kufanya ni kupiga mswaki kinywa chako mara mbili kwa siku.
Vilevile kuondoa mabaki ya chakula kati ya meno na fizi na meno mara kwa mara. Haya yanaweza kupunguza kuoza kwa meno na ugonjwa wa fizi.
Via:Bbc