Wanawake walivyopaza sauti kupinga ukeketaji Ethiopia
Wasichana wadogo nchini Ethiopia wanachukua msimamo wa kijasiri dhidi ya mila mbaya ya Ukeketaji (FGM).
Alipokuwa na umri wa miaka 18, Zekia aligundua kwamba wazazi wake walikuwa wakijitayarisha kwa siri kwa ajili ya dadake mkubwa kufanyiwa ukeketwaji.
“Kaka yangu alisikia kuhusu hilo na akajaribu kuwakataza, aliwakumbusha kuwa tabia hiyo imepigwa marufuku na akasema ingemweka kwenye matatizo mengi,” aliliambia, Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na uzazi UNFPA. “
Zekia alikuwa ameshuhudia kwa macho yake mchakato huo unavyoweza kusababisha maumivu. “Ninataja daima ugumu ambao mpwa wangu alipitia alipojifungua.”
Ukeketaji wa wanawake ni kitendo cha ukatili wa kijinsia na ukiukaji unaotambulika kimataifa wa haki za binadamu, unaweza kusababisha hali nyingi mbaya, ikiwa ni pamoja na fistula ya uzazi inayosababishwa na kujifungua kwa shida, maambukizi, kutokwa na damu nyingi, majeraha ya kisaikolojia, na hata kifo.
Wazazi wake walipokataa kumsikiliza kaka yake, kka yake huyo aliripoti kesi hiyo kwa mamlaka wa eneo hilo, Kizazi kizima, jamii yao imejitolea kwa kile kinachoshikiliwa kama mila; lakini mfululizo mpya wa sheria ndogo ndogo na kampeni za uelewa zinavunja fikra hii na kuchochea vijana kama Zekia kupinga.
UNFPA inakadiria kuwa duniani kote mwaka 2024, karibu wasichana milioni 4.4, zaidi ya 12,000 kwa siku wako katika hatari ya kukeketwa, utaratibu huo sio tu kwamba husababisha madhara ya kimwili na kiakili, lakini wasichana wengi hupoteza wiki za masomo wanapopata nafuu, na wengi zaidi hawarudi kabisa, hii inapunguza uwezo wao wa kielimu na nguvu kazi, ikipunguza uwezo wao wa kupata kipato na kuweka mizani ya haki kuwa nzito zaidi dhidi yao.
Shakira, 53, alivumilia masaibu ya kuhuzunisha alipofanyiwa Tohara (FGM) akiwa msichana mdogo. ..Shakira aliendelea kuwa mama wa watoto wa kike watano, wasichana watatu na kiume wawili.
Wakati ujao mzuri kwa wasichana wadogo
Kwa bahati nzuri kwa dada yake Zekia, hakuwa mmoja wao: Wakuu wa eneo hilo waliingilia kati na kusimamisha ibada hiyo isifanyike, na kuwaokoa dada wote wawili na kuwafanya kuwa miongoni mwa watu wa kwanza katika jamii yao kutofanyiwa kitendo hicho.
Ingawa hawakunyanyapaliwa na familia au marafiki, haikuwa jambo rahisi kwa wasichana hao, lakini kama mtetezi hai dhidi ya ukeketaji, Zekia alitumia ujuzi wake kuongeza ufahamu kuhusu hatari miongoni mwa wengine kote katika wilaya yake.
“Wanajamii wangu wameanza kufuata mfano, kuwaepusha binti zao na hilo.”
Kwa kiasi kikubwa vuguvugu la chinichini, linaloongozwa na walionusurika katika nchi kote ulimwenguni, wasichana leo wako karibu theluthi moja ya uwezekano wa kufanyiwa kitendo hicho ikilinganishwa na miaka 30 iliyopita.
Zekia alisema majadiliano na wanafunzi wenzake na walimu wa kike pia ni muhimu katika kubadilisha fikra “hakuna msichana hata mmoja katika shule yangu na kundi letu la umri wangu ambaye amefanyiwa hayo kama matokeo,” aliiambia UNFPA.
“Nazungumzia madhara katika maeneo ambayo wanawake wanakusanyika, kama vile kwenye vituo vya kuchotea maji, viwanda vya kusaga unga na masoko,” alisema, akiongeza kuwa wanaume na wavulana pia wanajiunga na baadhi ya mijadala.
Wengi wa walionusurika ambao Zekia amekutana nao sasa wanapinga, pamoja na ukiukaji wa wanawake, pia haki za binadamu kama vile ndoa za utotoni, ambayo ni ya kawaida katika eneo hilo.
Ni mtindo mwingine Zekia na dada zake wamedhamiria kubadilisha “ingawa ana zaidi ya miaka 18, dada yangu bado hajaolewa kwani anataka kumaliza shule ya sekondari, hili lingekuwa jambo lisilowezekana miaka michache iliyopita.” anasema.
“Na nimedhamiria kuendelea na masomo yangu pia na kuwa daktari siku moja”.
Shakira, 53, alivumilia masaibu ya kuhuzunisha alipofanyiwa Tohara (FGM) akiwa msichana mdogo.
Jitihada za kimfumo
Mpango wa Pamoja wa UNFPA-UNICEF unafanya kazi katika nchi 17 ili kutokomeza ukeketaji na umezindua mipango katika wilaya nne katika eneo la Kati la Ethiopia, Dalocha ina mojawapo ya viwango vya juu zaidi vya mila hiyo nchini Ethiopia, ambapo karibu asilimia 76 ya wanawake na wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 49 walifanyiwa hivyo mwaka 2000; kufikia 2016, hii ilishuka hadi zaidi ya asilimia 60.
Kufikia mwaka jana, Mpango wa Pamoja ulisaidia zaidi ya vikundi 11,000 vinavyofanya kazi dhidi ya ukeketaji duniani kote, ambapo asilimia 83 yalikuwa mashirika ya ndani yanayoshirikiana na vuguvugu zinazoongozwa na walionusurika na kutetea mabadiliko ya kisheria, kisiasa na muhimu zaidi mabadiliko ya kijamii.
Mojawapo ya vikundi hivi ni Ofisi ya Kikanda ya Masuala ya Wanawake na Watoto, ambayo inapambana na mila hatarishi pamoja na sekta za afya na elimu na vyombo vya kisheria. Nuritu Sirbar ni mkuu wa ofisi hiyo, anaeleza jinsi wanajamii yenye ushawishi mkubwa, wakiwemo viongozi wa dini na watendaji wa zamani, walivyojitokeza.
“Kuna maendeleo, sasa tunasajili wasichana wote katika shule ya chekechea na kufanya kazi na wazazi wao ili kuhakikisha kwamba hawapitii hilo, pia tunafanya kazi na vikundi vya vijana na shule, kuongeza ufahamu miongoni mwa wavulana na wanaume vijana pia,” Bi Sirbar alisema.
“Nilijua ni kwa nini tulilazimisha ukeketaji, lakini nilipoulizwa kwenye mkutano, sikuwa na jibu zuri la kutosha, Kwa mara ya kwanza, niligundua kwamba hatuwezi kutetea mila hiyo kwa kusema tu kwamba ni mila, vijana huuliza kwa nini na kutafuta jibu katika sayansi, si katika hadithi za kale,” alisema Simrimula Hamiza, Mzee katika jamii.
Na ingawa inaweza kuchukua muda kwa kizazi kipya kuibuka kikamilifu, “kuna mabadiliko angani.” Aliongeza Bi Sirbar.
Via:UN
Soma Zaidi hapa;