Fidia poda zenye kemikali ya talc zilizosababisha saratani ya ovari.
Johnson & Johnson imesema watalipa dola bilioni 6.5 ili kumaliza maelfu ya kesi nchini Marekani zinazodai kuwa poda zenye kemikali ya talc zilisababisha saratani ya ovari.
Mpango huo utasaidia J&J kusuluhisha kesi hizo kupitia kesi tatu za kampuni tanzu ya LTL Management.
Kutakuwa na kipindi cha miezi mitatu cha kupiga kura kwa wadai, kwa matumaini ya kufikia makubaliano juu ya madai yote ya sasa na yatakayokuja dhidi ya saratani ya ovari.
Takriban asilimia 99% ya kesi zinazohusiana na talc zilizowasilishwa dhidi ya J&J na kampuni tanzu zinatokana na saratani ya ovari.