SHINIKIZO LA DAMU, CHANZO NA TIBA YAKE
Nini maana ya shinikizo la damu?
Ni msukumo wa damu ulio juu kuliko inavyotakiwa.
japo Msukumo wa damu
huhitajika mwilini ili kusambaza chakula, oksijeni na kutoa uchafu ila usiwe juu kuliko kawaida.
Shinikizo la damu hupimwa kwa kutumia kifaa kinachoitwa Sphygmomanometer
CHANZO CHA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU
Shinikizo la damu husababishwa na nini?
Vitu vifuatavyo vinaweza kusababisha shinikizo la juu la damu:
- Uvutaji sigara
- Unene na uzito kupita kiasi
- Unywaji wa pombe
- Upungufu wa madini ya potassium
- Upungufu wa vitamin D
- Umri mkubwa
- Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin)
- Kushindwa kufanya kazi kwa kichocheo kiitwacho insulin N.k
Uanishaji wa shinikizo la damu
Presha ya kawaida (90-120/60-90)
Presha inayoelekea kupanda 120-139 80-89
Presha hatua ya 1 140-159 90-99
Presha hatua ya 2 160-179 100-109
Presha hatua ya 3 ≥180 ≥110
Shinikizo la damu/BP ni ugonjwa unaosumbuwa watu wengi sana duniani na hii ni kutokana na kutokujuwa ni nini hasa husababisha ugonjwa huu mwilini. Shinikizo la damu linaonekana kuwa ni ugonjwa wa kuishi kwa kufuata masharti.
Katika makala hii tutaona uhusiano mkubwa uliopo kati ya upungufu wa maji mwilini na ugonjwa huu, mwishoni utakuwa umeelewa sasa ni jinsi gani ilivyo rahisi kabisa kujiepusha na kujiponya ugonjwa huu. Endelea kusoma.
Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinasema tayari watu bilioni moja duniani kote, wanaathiriwa na shinikizo la juu la damu huku likisababisha mshtuko wa moyo (Heart Attacks), kupooza na kiharusi (Strokes).
Takribani watu milioni nane hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huu wa kupanda kwa shinikizo la damu.
DALILI ZA SHINIKIZO LA DAMU
- Maumivu ya kichwa (Haswa nyuma ya kichwa mara nyingi nyakati za asubuhi),
- Kuhisi hali ya Kuchanganyikiwa
- Kizunguzungu
- Kelele sikioni (Mvumo au Mazomeo masikioni)
- Kutoweza kuona vizuri au
Matukio ya kuzirai
- Uchovu/kujisikia kuchokachoka
- Mapigo ya moyo kwenda haraka
- Kutokuweza kuona vizuri
- Damu kutoka puani
Uonapo dalili hizi unapaswa kuwahi hospitali kupata vipimo.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.