TATIZO LA MAJI YA UZAZI KUWA MENGI KULIKO KAWAIDA(POLYHYRAMNIOS)
Tatizo la maji ya uzazi(amniotic fluid) kuwa mengi kuliko kawaida,ni tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama POLYHYRAMNIOS,
Ingawa tatizo hili huwapata wanawake wachache yaani asilimia 1% mpaka 2% tu ya ujauzito ambapo hugundulika baada ya vipimo kama ultrasound kufanyika, ila bado lipo na linatokea kwa baadhi ya wajawazito.
DALILI ZA TATIZO HILI LA MAJI YA UZAZI KUWA MENGI KULIKO KAWAIDA(POLYHYRAMNIOS) NI PAMOJA NA;
1. Mama mjamzito kushindwa kupumua au kukosa pumzi kabsa
2. Mama mjamzito kuvimba miguuni na kwenye kuta za tumbo
3. Mama mjamzito kuanza kusikia mkazo tumboni/tumbo kukaza sana au mgandamizo usio wakawaida tumboni
4. Mtoto kukaa vibaya tumboni yaani Malposition,mtoto kuanza kutanguliza matako badala ya kichwa yaani Breech presentation n.k
5. Mama mjamzito kuwa na tumbo kubwa sana kuliko kawaida N.K
CHANZO CHA TATIZO HILI LA POLYHYRAMNIOS NI PAMOJA NA;
- Mtoto kuzaliwa na matatizo mbali mbali ya kiuumbaji yaani Birth defects kama vile, matatizo ambayo huathiri mfumo mkuu wa fahamu(Central nervous system) au matatizo yanayoathiri mfumo wa chakula yaani Gastrointestinal track n.k
- Mama mjamzito kuwa na tatizo la Kisukari yaani maternal diabetes
- Tatizo la Twin-Twin transfusion, hili ni tatizo ambalo huhusisha mapacha hasa mapacha wa kufanana yaani IDENTICAL TWINS,ambapo pacha mmoja hupokea damu nyingi kuliko pacha mwingine
- Mtoto kuwa na tatizo upungufu wa seli hai nyekundu za damu(Red blood cells-RBC"s) mwilini au tatizo la upungufu wa damu mwilini yaani Fetal anemia
- Tatizo la damu ya mama na mtoto kutokuendana yaani mother and baby Blood incompatibilities
- Mama kupata maambukizi ya magonjwa mbali mbali kipindi cha Ujauzito n.k
MADHARA YA TATIZO LA POLYHYRAMNIOS NI PAMOJA NA;
• Mtoto kuzaliwa kabla ya wakati wake yaani Premature birth
• Mama mjamzito kupatwa na tatizo la Chupa ya uzazi kupasuka yaani Premature rupture of membrane(PROM)
• kondo la nyuma kuachia sehemu lilipojishikiza yaani Placental abruption
• Tatizo la cord ya mtoto kutokeza na kutangulia nje ya uke kabla ya mtoto kutoka yaani umbilical cord prolapse
• Mama mjamzito kujifungua kwa njia ya upasuaji yaani C-section delivery
• Mtoto kuzaliwa akiwa amefariki yaani still birth
• Mama kuvuja damu nyingi baada ya kujifungua kutokana na misuli ya tumbo la uzazi kushindwa kusinyaa na kurudi kwenye hali yake ya awali yaani uterine atony n.k
MATIBABU YA TATIZO HILI LA POLYHYRAMNIOS
- Endapo kiwango cha maji ya uzazi yaliyozidi(extra amniotic fluid) sio kikubwa sana,shida hii huweza kuisha yenyewe pasipo matibabu ya aina yoyote ile kwa mama mjamzito,
Ila endapo kiwango cha maji ya uzazi yaliyozidi ni kikubwa zaidi,basi matibabu mbali mbali huweza kufanyika kama vile;
✓ Kuvuta maji ya uzazi yaliyozidi yaani drainage of extra amniotic fluid
✓ Matibabu ya magonjwa kama kisukari(Diabetes) huweza kusaidia pia tatizo hili la POLYHYRAMNIOS kuisha lenyewe
✓ Matumizi ya dawa za kumeza yaani vidonge(Oral medications) kama vile INDOMETHACIN(Indocin),
Dawa hizi husaidia kupunguza uzalishwaji wa mkojo kwa mtoto,kisha kupunguza kiwango cha maji ya uzazi yaani amniotic fluid volume,
KUMBUKA; Dawa hizi haziruhusiwi kwa mama mjamzito ambaye ujauzito una umri wa zaidi ya wiki 31, kutokana na kuweza kuleta madhara mbali mbali kwa mtoto kama vile matatizo kwenye moyo yaani Fetal heart problems n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.