Uzalishaji wa chanjo ya Mpox barani Afrika wajadiliwa
Kampuni ya dawa ya Afrika, Aspen Pharmacare, inafanya mazungumzo na washirika wake kuhusu uzalishaji wa chanjo za Mpox katika viwanda vyake, alisema Mkurugenzi Mtendaji Stephen Saad alipoongea na Reuters Jumanne.
Bara la Afrika lipo chini ya shinikizo la kudhibiti mlipuko wa maambukizi hayo hatari, ambao Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kuwa dharura ya afya ya umma duniani mnamo katikati ya Agosti, baada ya aina mpya ya virusi kuanza kusambaa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwenda nchi jirani.
Nchi kumi na tatu za Afrika zimeripoti zaidi ya kesi 22,800 za Mpox na vifo 622 mwaka huu, kwa mujibu wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (Africa CDC) mwezi uliopita.
“Tunaongea na watu,” alisema Saad bila kutaja kampuni zinazohusika, akiongeza kuwa Aspen ina uwezo wa kuzalisha chanjo hizo na wanahisi wako tayari kufanya uzalishaji huo.
Hata hivyo, Aspen imetoa masharti mawili ili kuepuka hali ya kukosa kazi kama ilivyotokea wakati walipotengeneza chanjo za COVID-19 ambazo hazikuhitajika kwa kiasi kikubwa. Kwanza, kampuni inataka ahadi ya kiasi cha maagizo yatakayofanywa, na pili, inahitaji kufidiwa gharama za kuhamisha teknolojia ya uzalishaji wa chanjo hizo kwenye kiwanda chao.
Mpox, ambayo inaweza kusambaa kupitia mawasiliano ya karibu, kwa kawaida huwa si hatari sana lakini inaweza kusababisha vifo kwa nadra. Inasababisha dalili kama za mafua na majipu yenye usaha mwilini.
Zaidi ya watoto 160,000 wachanjwa, lengo ni watoto 640,000
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti leo Jumanne Septemba 3 kwamba watoto 161,030 walio na umri wa chini ya miaka kumi wamechanjwa katikati mwa Gaza wakati wa siku mbili za kwanza za kampeni ya chanjo inayoongozwa na Umoja wa Mataifa, hivyo kuvuka lengo la awali la watoto 156,000.
Idadi hii inawakilisha takriban robo ya jumla ya watu watakaofikiwa, watoto 640,000.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa X akisema, “timu zetu zimejizatiti kuhakikisha hakuna mtoto anayekosa (kuchanjwa), licha ya ufurushaji unaoendelea.”
Tweet URL
Saa za kutoshambuliana
Hata hivyo, mwakilishi wa WHO kwa Maeneo ya Palestina Yanayokaliwa, Rik Peeperkorn, akizungumza kutoka Gaza leo amesema watahitaji siku moja zaidi ili kukamilisha uchanjaji kikamilifu eneo la kati la Gaza.
Amesema siku ya tatu ya uchanjaji imeendelea wakati wa mapumziko ya kutoshambuliaana kila siku kwa saa nane ziliyokubaliwa na jeshi la Israel na wapiganaji wa Hamas (saa kumi na mbili asubuhi hadi saa tisaa alasiri).
Eneo la kusini
Peeperkon ameeleza kuwa timu za chanjo zitahamia eneo kubwa la kusini siku ya Alhamisi kwa siku nyingine tatu na kuna uwezekano mkubwa wa siku ya nne, kabla ya kuelekea ukanda wa kaskazini.
"Wiki nne baadaye, mchakato huo utarudiwa kwa awamu ya pili ya chanjo." ameongeza.
Kufikia sehemu ya kaskazini mwa Ukanda huo bado kunatia wasiwasi, kwani WHO imejaribu kutuma watu wake kaskazini katika wiki mbili zilizopita ili kuzipatia hospitali vifaa muhimu vya matibabu.
"Kati ya makundi nane au tisa yaliyopangwa, ni matatu au manne tu ndio yaliweza," anasema, akiongeza kwamba walituma timu ya matibabu ya dharura katika hospitali ya Indonesian na daktari wa watoto katika hospitali ya Kamal Adwan, pamoja na dawa na vifaa vingine.
"Kati ya makundi nane au tisa yaliyopangwa, ni matatu au manne tu ndio yaliweza," anasema.
Safari ya kurudi kwenye kituo ilihusisha kusubiri ruhusa kwa saa saba ili kuendelea hadi kufika mahali pa kupumika, na saa 2.5 za ziada kufikia kituo cha ukaguzi.
Asilimia 90
Kwa mujibu wa WHO, angalau asilimia 90 ya watoto wa Kipalestina wanahitaji kupewa chanjo ili kampeni hiyo iwe na ufanisi na kuzuia kuenea kwa polio ndani ya Gaza na duniani kote.
Ukanda wa Gaza ulikuwa na kiwango cha juu cha chanjo kwa watu wote kabla ya mzozo kuanza Oktoba 2023.
Kutokana na athari za vita, uchanjaji wa kawaida ulishuka kutoka asilimia 99 mwaka 2022 hadi chini ya asilimia 90 katika robo ya kwanza ya mwaka 2024, na kuongeza hatari ya magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa watoto, ikiwa ni pamoja na polio.
Alipoulizwa kama itawezekana kutathmini masuala mengine makubwa ya kiafya, kama vile utapiamlo wa watoto, wakati timu za chanjo zikifanya kazi, Peeperkorn amesema hakuna uwezo wa kufanya hivyo.
Watoto waliochanjwa wanarudi kwenye eneo la vita
Wakati mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yakikaribisha usitishaji mapigano katika maeneo maalum ili kuruhusu kampeni kubwa ya chanjo ya polio, yanasisitiza haja ya dharura ya kuachiliwa mara moja kwa mateka wote waliosalia na kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza.
"Watoto hawa wakishachanjwa, watarejea katika maeneo ambayo tunafikiri yatapigwa mabomu tena wiki ijayo," anaonya James Elder, msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF).
"Hakuna kitu kuhusu hilo ambacho kinapaswa kukubaliwa kama hali ya kawaida," ameendelea. "Na nadhani kila mtu sasa anakubali kwamba mazungumzo ya kusitisha mapigano ni mazungumzo ya kutufanya tuendeleea.
Via:UN
kampeni ya utoaji chanjo kwa watoto yaanza huko Gaza
WHO
Kampeni ya Umoja wa Mataifa ya chanjo ya polio inaendelea katikati mwa Gaza
Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA Phillipe Lazzarini amesema awamu ya kwanza ya zoezi kubwa la kampeni ya utoaji chanjo ya polio kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 10 limeanza rasmi hii leo huko katikati mwa ukanda wa Gaza, huku akieleza kuwa kampeni hii inakimbizana na muda ili iweze kufikia watoto 600,000 katika ukanda huo.
Katika taarifa yake aliyoichapishwa kwenye mtandao wa X hii leo Lazzarini amesema mama mmoja amemueleza anahisi ahueni baada ya mtoto wake kupata matone mawili ya dozi ya chanjo ya polio katika kliniki ya UNRWA.
Hata hivyo kiongozi huyo wa UNRWA amesisitiza kuwa ili kampeni hiyo iweze kufanikiwa, pande zote katika mzozo unaoendelea huko Gaza ni lazima ziheshimu sitisho la muda la mapigano katika ukanda huo.
“Kwa ajili ya watoto wa ukanda huu, ni wakati wa kuwa na sitisho la kudumu la mapigano,” aliongeza Lazzarini.
Kwa upande wake, Sam Rose, Kaimu Mkurugenzi wa Operesheni za UNRWA huko Gaza, kupitia chapisho kwenye mtandao wa X ameeleza kwamba, timu za mawakala zitawafikia maelfu ya watoto na kuwapatia chanjo ya polio katika kliniki, vituo vya afya na kupita kutoka hema hadi hema katika Ukanda mzima.
Amesisitiza kuwa UNRWA itatoa chanjo hadi kwa nusu ya watoto hao, na takriban wafanyakazi 1,100 wa shirika hilo watashiriki katika kampeni hiyo inayofanywa na Wizara ya Afya ya Palestina kwa ushirikiano na UNRWA, WHO na UNICEF.
Chanjo bora zaidi ni amani
Akizungumzia kuhusu kuanza kwa zoezi hilo la utoaji chanjo kwa watoto walioko Gaza, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema watoto hao wa Gaza wanapokea chanjo hiyo inayohitajika zaidi.
Hata hivyo Dkt.Tedros amesema suluhisho la kweli ni amani “Mwisho wa wote, chanjo bora zaidi kwa watoto hawa ni amani”
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kanda wa Shirika la Afya Duniani kwa Mashariki ya Mediterania, Dkt. Hanan Balkhi, amesema kuwa kuna haja ya chanjo hiyo kufikia angalau asilimia 90 ya wanaotarajiwa kupatiwa.
“Shukrani nyingi kwa pande zote zinazohakikisha usalama wa wafanyakazi wa afya, watoto na familia katika nyakati hizi ngumu”.
Nalo shirika la Umoja wa Mataiafa linaloshughulikia masuala ya watoto UNICEF limesisitiza kuwa pande zote lazima ziheshimu vipindi vya sitisho la mapigano kwa sababu za kibinadamu lililo bainishwa kwa kila eneo wakati wa kampeni hiyo ya utoaji chanjo.
Kovu la Begani baada ya Mtoto kupata chanjo, na nini cha kufanya kama KOVU halijatokea,
Chanjo ya kuzuia ugonjwa wa Kifua Kikuu Maarufu kama BCG ndyo hutoa KOVU kwenye bega la Mtoto,
chanjo hii hutolewa kwa njia ya sindano bega la kulia, na huchomwa mara tu baada ya mtoto kuzaliwa au mara ya kwanza anapofika kliniki kama hakupewa baada ya kuzaliwa,
Endapo KOVU halijatokea Begani, chanjo hii hurudiwa tena baada ya miezi 3,
• • • • •
CHANJO ZA MTOTO TOKA ANAZALIWA MPAKA ANAPOFIKIA UMRI WA MIAKA 5
1. Chanjo ya kuzuia ugonjwa wa Kifua Kikuu Maarufu kama BCG
chanjo hii hutolewa kwa njia ya sindano bega la kulia, na huchomwa mara tu baada ya mtoto kuzaliwa au mara ya kwanza anapofika kliniki kama hakupewa baada ya kuzaliwa,
Endapo KOVU halijatokea Begani, chanjo hii hurudiwa baada ya miezi 3
2. Chanjo ya Kuzuia ugonjwa wa Kupooza Yaani POLIO
Chanjo hii hutolewa kwa njia ya matone mdomoni mara tu baada ya mtoto kuzaliwa au mara ya kwanza anapofika kliniki kama hakupewa baada ya kuzaliwa,
Halafu hurudiwa baada ya mwezi 1, 2, na 3.
3. Chanjo ya PENTAVALENT(DTP)
chanjo hii huzuia magonjwa matano yaani; Donda koo,kifaduro,pepopunda,homa ya ini, na homa ya manjano
chanjo hii hutolewa kwa njia ya sindano ya paja la Kushoto na hutolewa mtoto akiwa na umri wa mwezi 1, hurudiwa mwezi 2 na 3.
4. Chanjo ya PCV13
Chanjo hii husaidia kuzuia ugonjwa wa Pneumonia kwa mtoto
chanjo hii hutolewa kwa njia ya sindano ya paja la Kulia na hutolewa mtoto akiwa na umri wa mwezi 1, hurudiwa mwezi 2 na 3.
5. Chanjo ya ROTARIX
chanjo hii ni kwa ajili ya kuzuia ugonjwa wa Kuharisha kwa mtoto ambao husababishwa na RotaVirus,
na hutolewa kwa mtoto kuanzia wiki ya 6 na wiki ya 10 .
6. Chanjo ya kuzuia ugonjwa wa SURUA
Chanjo hii hutolewa mtoto akiwa na umri wa miezi 9 na miezi 18
7. VITAMIN A
Mtoto hupata vitamin A supplements akiwa na umri wa kuanzia miezi 6, 12,18,24,30,36,42 na 54
8. Dawa za MINYOO
Dawa za minyoo huanza kutolewa mtoto akiwa na umri wa kuanzia miezi 12,18,24,30,36,42 na 54
kwa Maelezo Zaidi na Msaada kuhusu kusoma KADI yako Ya KLINIKI Bofya hapa..!!
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Viongozi wa dunia pamoja na wawakilishi wa mashirika ya afya na makampuni ya dawa wamejumuika pamoja siku ya Alhamisi mjini Paris, Ufaransa katika mkutano wa kilele unaojadili masuala ya chanjo.
Katika mkutano huo, kumetangaza ufadhili wa dola bilioni 1.2 zitakazowezesha kuzalisha chanjo huko Afrika, bara ambalo linakabiliwa na matatizo mengi ya kiafya ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa magonjwa ya milipuko kama kipindupindu.
Mbali na viongozi wa Magharibi, mkutano huo umehudhuriwa pia na viongozi kutoka nchi kadhaa za Kiafrika kama Botswana, Rwanda, Senegal, Ghana, Mataifa mengine yamewakilishwa na mawaziri.
Katika hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kitendo cha kupiga jeki utengenezaji wa chanjo barani humo, itakuwa hatua muhimu kuelekea kuanzishwa kwa soko la kweli la chanjo Afrika.
Macron ameendelea kusema kuwa robo tatu ya fedha hizo zitafadhiliwa na mataifa ya Ulaya. Ujerumani itachangia dola bilioni 318 kama alivyoeleza Kansela Olaf Scholz katika ujumbe wa video. Ufaransa itatoa dola milioni 100, Uingereza dola milioni 60, huku wafadhili wengine wakiwa ni pamoja na Marekani, Canada, Norway, Japan na Wakfu wa Bill na Melinda Gates.
Kauli za viongozi mbalimbali wakiwemo wa Afrika
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat aliuambia mkutano huo kwamba mpango huo unaweza kuwa kichocheo cha kukuza sekta ya dawa barani Afrika na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi wanachama. Mahamat amesema Afrika huagiza nje ya bara hilo asilimia 99 ya chanjo zake na kwa gharama kubwa.
Janga la UVIKO-19 liliweka bayana hali ya kutokuwepo usawa katika usambazaji wa chanjo ulimwenguni, kwani nchi tajiri zenye makampuni mengi makubwa ya dawa zilijipatia dozi nyingi za chanjo na kuiacha Afrika ikiwa nyuma. Mpango huo mpya unalenga kuanzisha uzalishaji wa chanjo barani Afrika ili kuliwezesha bara hilo kuwa na uhuru zaidi na kuepusha kujirudia kwa hali iliyoshuhudiwa wakati wa janga la corona.
Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza David Cameron, aliuambia mkutano huo kwamba wakati kutakapotokea janga jingine, na hata kama viongozi katika nchi tajiri za Magharibi watakuwa na nia njema kama malaika, bado kutakuwepo shinikizo la kujihifadhia chanjo kwa ajili ya watu wetu, na kwamba hilo halitazuilika kila wakati.
Kuibuka tena kwa ugonjwa la kipindupindu hivi karibuni katika maeneo mengi ya Afrika, kumeonyesha hitaji la kuwepo wazalishaji zaidi wa chanjo ndani ya Afrika. Kwa sasa, ni kampuni moja tu duniani ya EuBiologics ya Korea Kusini ndio hutengeneza dozi za chanjo kwa bei nafuu ili kukabiliana ugonjwa huo hatari.
Macron amesema mlipuko wa kipindupindu kwa sasa unaathiri karibu nusu ya Afrika huku akitoa wito kwa kuufanya ugonjwa huo kutokomezwa kabisa. Alitangaza pia msururu wa uzalishaji wa chanjo za kipindupindu utakaozinduliwa barani Afrika na kampuni ya biopharmaceutical ya Afrika Kusini ya Biovac.
Muungano wa Gavi unaoyajumuisha mashirika mbalimbali yenye jukumu la kusaidia kusambaza chanjo za zaidi ya magonjwa 20 kwa nchi maskini , ulikuwa mmoja wa waandaaji wa Jukwaa hilo la Kimataifa kuhusu uhuru na ubunifu wa Chanjo. Katika kongamano hilo, muungano wa Gavi ulitangaza kuwa unalenga kukusanya dola bilioni 9 ili kufadhili programu zake za chanjo kuanzia mwaka 2026 hadi 2030.
Mwenyekiti wa Gavi Jose Manuel Barroso amesema kitendo cha kuwapa chanjo watoto milioni moja tangu mwaka 2000 ni mafanikio ya ajabu, na kwamba mtoto anayezaliwa zama hizi, anaweza kufikisha kwa urahisi miaka mitano kuliko hapo awali katika historia.
Hata hivyo, Barroso ameongeza kusema kuwa bado kuna mamilioni ya watoto ambao hawajapata chanjo dhidi ya ugonjwa wowote huku mamia ya mamilioni ya wengine wakihitaji kupatiwa chanjo zaidi.
Hadi sasa, asilimia mbili tu ya chanjo zinazotolewa barani Afrika ndizo hutengenezwa katika bara hilo. Umoja wa Afrika unalenga kuongeza idadi hiyo hadi kufikia asilimia 60 ifikapo mwaka 2040.
(Chanzo: AFP)
Putin kuja na Chanjo ya Saratani hivi karibuni.
RAIS wa Urusi, Vladimir Putin amesema wanasayansi nchini humo wanakaribia kutengeneza chanjo ya saratani ambayo itaanza kupatikana hivi karibuni.
Akizungumza jana jioni katika kituo kimoja cha televisheni nchini humo Putin amesema: “tumekaribia sana kuundwa kwa kinachojulikana kama chanjo ya saratani na dawa za kinga za kizazi kipya”.
“Natumai kwamba hivi karibuni zitatumika kwa ufanisi kama njia za matibabu ya mtu binafsi,” aliongeza, akizungumza katika kongamano la Moscow juu ya teknolojia ya siku zijazo.
Putin hakutaja aina gani za saratani ambazo chanjo zilizopendekezwa zingelenga, wala jinsi gani zitafanya kazi.
Idadi ya nchi na makampuni yanafanyia kazi chanjo ya saratani. Mwaka jana, Serikali ya Uingereza ilitia saini makubaliano na kampuni ya BioNTech yenye makao yake Ujerumani kuzindua majaribio ya kliniki yanayotoa “matibabu ya kibinafsi ya saratani”, yanayolenga kufikia wagonjwa 10,000 ifikapo 2030.