Vituo vya Marekani vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) siku ya Alhamisi vilitoa tahadhari na kuwataka watoa huduma za afya kuongeza chanjo ya mafua, COVID-19 na virusi vya kupumua vya syncytial (RSV).
Mdhibiti wa afya alisema kuwa kuwepo kwa viwango vya chini vya chanjo, pamoja na kuongezeka kwa ugonjwa wa kupumua, kunaweza kusababisha ugonjwa mbaya zaidi na kuongezeka kwa uhitaji wa huduma za afya katika wiki zijazo.
Watoa huduma za afya wanapaswa kupendekeza dawa za kuzuia virusi vya mafua na COVID-19 kwa wagonjwa wote wanaostahiki, haswa wazee na watu walio katika hali fulani ya Kimatibabu, CDC ilisema.
Katika wiki nne zilizopita, Idadi ya watu kulazwa hospitalini kulingana na umri iliongezeka kwa asilimia 200% kwa mafua, 51% kwa COVID-19, na 60% kwa RSV, kulingana na data za CDC.
Kulikuwa na dozi milioni 7.4 za chanjo ya mafua ambazo ni chache kwa ajili ya watu wazima katika maduka ya dawa na ofisi za madaktari ikilinganishwa na msimu wa homa wa Mwaka 2022-2023.