Fahamu hapa Madhara ya gesi tumboni na chanzo chake
Sababu za gesi tumboni huweza kuwa sababu za kawaida kama vile kumeza hewa hadi sababu za hatari zaidi kama vile kuwa na ugonjwa wa saratani ya utumbo.n.k
Hata hivyo, watu wenye gesi isiyoisha au inayozidi kuwa mbaya huenda wakahitaji msaada wa kitiba kwa sababu ya hali fulani ya msingi.
Makala hii inaeleza dalili za gesi tumboni na sababu zake mbalimbali. Pia inaainisha chaguzi tofauti za matibabu kwa tatizo la gesi tumboni na hutoa maelekezo kuhusu wakati wa kumuona daktari.
Dalili za gesi tumboni
Kulingana na taasisi inayohusika na maswala ya ugonjwa wa kisukari,mfumo wa umeng’enyaji chakula pamoja na ugonjwa wa figo “National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases (NIDDK)”, Hizi hapa ndyo dalili kuu za tatizo la gesi tumboni;
- Mtu kujamba mara kwa mara
- Kuhisi hali ya tumbo kujaa
- Kupata maumivu ya tumbo
- Tumbo kuvuruga(discomfort)
- Tumbo kuongezeka ukubwa(Size)
Na kwa baadhi ya watu hupata dalili hizi pia;
- Kiungulia
- Kuharisha
- Kukosa choo n.k
Madhara ya gesi tumboni
Haya hapa ni baadhi ya madhara ambayo huweza kusababishwa na tatizo la tumbo kujaa gesi;
1. Kupata Maumivu ya tumbo, tatizo la gesi tumboni huweza kusababisha mtu kupata maumivu ya tumbo,
na endapo maumivu haya ni makali na yanadumu kwa muda mrefu(Prolonged abdominal pain) hakikisha unawahi hospital kwa ajili ya vipimo Zaidi.
2. Kukosa choo au kupata choo kigumu
Pia tatizo la gesi tumboni huweza kuambatana na matatizo mengine kama vile; mtu kukosa choo kabsa au wakati mwingine kujisaidia choo kigumu.
3. Mtu kujamba sana, kila wakati(mara kwa mara)
4. Kwa baadhi ya Watu wenye shida ya gesi tumboni huharisha pia wakati wa kujisaidia
5. Kupata kiungulia cha Mara kwa mara
6. Na baadhi hupata shida ya kichefuchefu na kutapika,
endapo unatapika mara kwa mara au mfululizo wahi hospital kwa ajili ya Vipimo Zaidi.
7. Wapo watu pia wakipata shida ya gesi tumboni hupata maumivu ya Kifua(chest pain)
8. Ukiona unashida ya gesi tumboni halafu unajisaidia kinyesi chenye damu, hakikisha unawahi kwenye Vipimo.
Chanzo cha Gesi tumboni
Zipo sababu mbali mbali za tatizo la gesi tumboni, na sababu hizo ni pamoja na;
– Kumeza hewa ndani(Swallowing air),
Mara nyingi,watu humeza hewa wakati wa kula, na hii inaweza kufanya tumbo au sehemu ya juu ya tumbo kujisikia hali ya kujaa.
Ndyo maana,pia unashauriwa usiongee wakati wa kula, tabia hii itakufanya umeze chakula pamoja na hewa ndani.
Kwa ujumla,Vitu hivi huongeza hatari ya wewe kumeza hewa ndani;
- Kuongea wakati wa kula
- Kula au kunywa haraka sana
- Kutafuna bigG(gum)
- Kunyonya pipi ngumu
- Kunywa vinywaji vyenye kiwango kikubwa cha wanga(Carbonated drinks) kama vile Soda,beer n.k
- Uvutaji wa Sigara n.k
– Kuwa na tatizo la acid Reflux au Gastroesophageal reflux disease (GERD)
Tatizo hili ni miongoni mwa matatizo ambayo huweza kusababisha shida ya gesi tumboni.
Soma Zaidi hapa: Tatizo la Acid reflux,chanzo,dalili na madhara yake
– Kula baadhi ya vyakula vyenye Gesi
Kula baadhi ya vyakula vyenye gesi sana huweza kuwa chanzo cha tatizo la gesi tumboni, vyakula hivo ni pamoja na;
- Maharage
- cabbage
- Baadhi ya mboga za majani
- Vitunguu
- Maziwa pamoja na vitu vyenye maziwa ndani yake kama vile yogurt n.k
– Kuwa na bacteria wengi kupita kiasi(Bacterial overgrowth)
Ukuaji wa bacteria wengi kupita kiasi tumboni au kwenye utumbo mdogo huweza kupelekea mtu kupata shida ya tumbo kujaa gesi.
– Kuwa na tatizo la Food intolerances
Wakati mwingine tumbo kujaa gesi huweza kutokana na shida ya Food Intolerances,
Food Intolerances; ni pale ambapo mwili wako unashindwa kumeng’enya baadhi ya vyakula vizuri mfano;
- Unashindwa kumeng’enya sukari aina ya lactose inayopatikana kwenye maziwa au bidhaa zenye maziwa, hii kwa kitaalam tunaita Lactose intolerance n.k
– Sababu hizi pia huweza kuwa chanzo cha Gesi tumboni;
- Tatizo la kukosa choo au kipata choo kigumu kwa muda mrefu(chronic constipation)
- Tatizo la vidonda vya tumbo
- Tatizo la hernias
- Kuziba kwa utumbo mdogo(intestinal blockages)
- Kuwa na Saratani ya utumbo mpana(colon cancer) n.k
Matibabu ya Gesi tumboni
Unaweza kupata matibabu sahihi ya tatizo la gesi tumboni baada ya kufahamu chanzo husika,
Ila kwa ujumla kuna dawa za kutibu shida hii ikaisha kabsa. Pamoja na dawa,lakini pia ni muhimu kuzingatia baadhi ya vitu kama vile;
✓ Kutafuna chakula vizuri
✓ Kuepuka kuongea wakati wa kula
✓ Kutokula au kunywa haraka haraka
✓ Kuepuka vyakula au vinywaji vyenye kiwango kikubwa cha carbohydrates
✓ Kuepuka kabsa kuvuta Sigara n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.