Madhara ya kuwepo kwa usaha kwenye mapafu
Baada ya kufanya vipimo ukagundulika una shida ya usaha kwenye mapafu, ni madhara gani unaweza kukutana nayo?
Tatizo la usaha kwenye mapafu, ni tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Empyema,
Empyema; ni mkusanyiko wa usaha kwenye eneo katikati ya mapafu na kuta za ndani za kifua(pleural space).
Tatizo hili hujulikana kama Empyema, lakini majina mengine ni kama vile;Empyema – pleural; Pyothorax; Pleurisy – purulent.
Chanzo cha Usaha kwenye Mapafu
Usaha kwenye Mapafu unasababishwa na nini?
Tatizo hili la Usaha kwenye mapafu husababishwa na maambukizi(infections) ambayo husambaa kutoka kwenye mapafu na kupelekea mkusanyiko wa Usaha kwenye eneo katikati ya mapafu na kuta za ndani za kifua(pleural space).
Vitu hivi huongeza hatari ya Mtu kupata tatizo la Usaha kwenye Mapafu;
1. Tatizo la pneumonia ambalo hutokana na maambukizi ya Bacteria(Bacterial pneumonia)
2. Tatizo la TB(Tuberculosis)
3. kufanyiwa upasuaji wa kifua
4. Kuwa na jipu au majipu kwenye Mapafu(Lung abscess)
5. Kupata jeraha au kuumia eneo la kifuani
6. Na kwa nadra sana, shida ya usaha kujikusanya kwenye mapafu huweza kutokana na procedure inayojulikana kama thoracentesis.
procedure hii huhusisha mtu kutobolewa na sindano eneo la kufuani ili kutoa majimaji(fluid) kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.
Madhara ya kuwepo kwa usaha kwenye mapafu
Kama unashida ya Usaha kwenye mapafu unaweza kupata madhara haya;
– Kupata Maumivu makali ya kifua(Chest pain), ambayo huzidi sana wakati wa kuvuta hewa ndani
– Mtu kukohoa kikohozi kikavu sana(Dry cough)
– Kuvuja jasho kupita kiasi hasa wakati wa Usiku
– Kupata homa za mara kwa mara na mwili kutetemeka sana
– Mtu kukosa pumzi kabsa
– Uzito wa mwili kupungua kwa kasi sana
– Mwili kuchoka sana kupita kiasi
– Mwili kuishiwa na nguvu kabsa n.k
Vipimo vinavyoweza kufanyika
vipimo ambavyo huweza kufanyika ili kugundua tatizo hili ni pamoja na;
- Chest x-ray
- CT scan ya Kifua
- Thoracentesis
- Pleural fluid analysis
Matibabu ya Tatizo la Usaha kwenye Kifua
Kitu cha kwanza ni kutibu maambukizi(Infections) yanayosababisha mkusanyiko wa usaha huu, pamoja na matibabu mengine,
Hivo kwa Ujumla mambo haya huweza kufanyika kwa mgonjwa mwenye shida ya Usaha kwenye mapafu;
✓ Kuwekewa mpira na kuvuta usaha wote ndani ya mapafu au kifua
✓ Kupewa dawa jamii ya antibiotics ili kudhibiti maambukizi
✓ Ikiwa una matatizo ya kupumua, unaweza kuhitaji upasuaji ili kusaidia mapafu yako kupanuka vizuri.n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.