Fahamu Aina ya dawa za macho pamoja na Matumizi yake
Dawa katika sehemu hii ni pamoja na zile ambazo hufanya kazi kwenye macho, na kawaida hutolewa kama matone ya macho(eye-drops) au mafuta(ointments).
Kuna aina nyingi tofauti – tofauti za dawa ambapo hutumika kwenye matibabu ya maambukizi kwenye macho, kwa mfano;
- chloramphenicol,
- fusidic acid,
- Pamoja na ciprofloxacin.
Shida ya Macho makavu inaweza kutibiwa kwa urahisi kwenye duka la dawa kwa kutumia dawa kama vile hypromellose na carbomer, muulize mfamasia au daktari kwa ushauri Zaidi, au tuwasiliane hapa @afyaclass.
Aina ya dawa za macho
Tuchambue hapa Baadhi ya Aina ya dawa za Macho;
1. Timolol Maleate Ophthalmic Solution
Dawa hii ni Nzuri sana kwa Watu wenye tatizo la Presha ya macho au kwa kitaalam hufahamika kama Ugonjwa wa glaucoma.
Glaucoma husababishwa na shinikizo la damu kuongezeka ndani ya jicho na matibabu kama vile latanoprost na timolol huweza kutumika.
2. Dawa ya Acetazolamide (Diamox)
Acetazolamide ni dawa kwa ajili ya glaucoma Pia.
3. Acetylcysteine(Ilube)
Dawa hii ni kwa ajili ya tatizo la macho kuwa makavu yaani “dry eyes”
4. Aciclovir eye ointment
Dawa hii hutumika kwenye macho kwa ajili ya maambukizi yanayosababishwa na herpes simplex virus.
5.Hypromellose Eye drops
Dawa hii ya macho hutumika kwa mtu mwenye tatizo la macho kuwa makavu au Usumbufu wowote wa macho unaotokana na kupungua kwa mtiririko wa machozi(tear flow),
Pia inaweza kusaidia kuzuia uharibifu wa macho kutokana na baadhi ya magonjwa.
6. Antazoline pamoja na xylometazoline eye drops (Otrivine-Antistin)
Hapa ni mchanganyiko wa dawa mbili Antazoline na Xylometazoline ambapo kwa pamoja tunaita Otrivine-Antistin.
Dawa hii huweza kuwa kama vasoconstrictor ambapo husaidia kupunguza shida ya macho kuwa mekundu(reduces eye redness).
Kumbuka: Usitumie dawa hizi pasipo maelekezo ya kina kutoka kwa Wataalam wa afya. Au kwa ushauri Zaidi, tuwasiliane hapa @afyaclass.
7. Apraclonidine eye drops (Iopidine)
Dawa hii hutumika kusaidia kushusha shinikizo la damu kwenye macho, hivo inafaa kwa mtu mwenye ugonjwa wa presha ya macho(glaucoma).
8. Atropine eye drops (Minims Atropine)
Dawa hii mara nyingi hutumiwa na Wataalam wa macho wakati wanafanya uchunguzi wa macho(eye examination),
Hii ni kutokana na sifa yake ya kuweza kutanua(dilate/enlarge) pupil kwenye jicho na kuifanya Lensi kufa ganzi kwa muda
(It is used to dilate (enlarge) the pupil of the eye and to temporarily paralyse the lens so that your doctor can examine your eye(s)).
9. Azelastine eye drops (Optilast)
Dawa hii ya Azelastine eye drops hutumika kwa mtu mwenye mzio au allergies mbali mbali za macho.
10.Azithromycin eye drops (Azyter)
Dawa hii ya macho huweza kutumika kutibu maambukizi mbali mbali ya bacteria kwenye macho ikiwemo maambukizi ya bacteria kwa Wazee pamoja na watoto toka wanazaliwa mpaka wenye umri wa miaka 17.
Maambukizi mbali mbali ya bacteria ni pamoja na;
- Purulent bacterial conjunctivitis;
- trachoma conjunctivitis ( haya ni maambukizi kwenye macho kutokana na bacteria wanaojulikana kama Chlamydia trachomatis)
11. Betamethasone eye drops (Betnesol, Vistamethasone)
Dawa hii ya macho huweza kutumika kutibu hali Zozote zinazosababisha uvimbe wa macho(short-term inflammatory eye conditions).
Kwa sababu dawa hii ina corticosteroid(steroid’) huweza kutumika kupunguza hali ya Uvimbe kwenye macho pamoja na wekundu kwenye macho(It helps relieve inflammation, redness and irritation).
12. Betaxolol eye drops(Betoptic)
Dawa hii ya macho hutumika kwa watu wenye ugonjwa wa Presha ya macho(glaucoma).
Dawa Zingine za Ugonjwa wa Presha ya macho ni pamoja na dawa kama vile;
- Brimonidine eye drops (Alphagan, Brymont).
- Brinzolamide eye drops (Azopt)
- Dorzolamide eye drops(Eydelto, Trusopt, Vizidor)
- Carteolol eye drops (Ocupress)
- Pilocarpine eye drops for acute glaucoma (Minims Pilocarpine) n.k
13. Chloramphenicol eye drops (Brolene, Golden Eye)
Dawa hii hutumika kutibu maambukizi mbali mbali ikiwemo ya bacteria kwenye macho
14. Ciprofloxacin eye preparations (Ciloxan)
Hii pia ni dawa ya macho ambayo hutibu baadhi ya maambukizi ya bacteria.
15. Dexamethasone eye drops (Maxidex, Dexafree, Dropodex)
Hii ni dawa ya macho ambayo hutumika kutibu kuvimba kwa macho(Inflammation), kutokana na mzio au allergies mbali mbali pamoja na hali kama vile;
Kuunguzwa na kemikali au joto(chemical and thermal burns).
Hivo kama una hali kama vile za allergies mbali mbali kwenye macho, hii pia ni nzuri.
16.Diclofenac eye drops (Voltarol Ophtha)
Diclofenac eye drops ni dawa ya macho ambayo hutumika kuondoa maumivu pamoja na hali ya kuvimba ambako huweza kutokana na sababu kama vile upasuaji wa jicho/macho,
mfano dawa hii ya Diclofenac eye drops huweza kutumika kuondoa maumivu na hali ya uvimbe baada ya mtu kufanyiwa upasuaji wa kutibu Mtoto wa jicho(cataract surgery).
17. Gentamicin eye drops
Dawa hii ya macho hutumika kutibu maambukizi ya bacteria kwenye jicho pamoja na ngozi kuzunguka macho, maambukizi hayo ya bacteria ni kama vile; blepharitis, conjunctivitis.
Pia hutumika kuzuia maambukizi kwenye jicho au macho baada ya mtu kuumia jichoni/macho au baada ya kufanyiwa Upasuaji wa macho.
18.Loteprednol eye drops (Lotemax)
Hii ni dawa ya macho kwa watu wenye shida ya kuvimba(Inflammation)
19. Moxifloxacin (Moxivig)
Hii ni kwa ajili ya maambukizi mbali mbali machoni.
20. Prednisolone eye drops
Hii ni dawa ya Macho ambayo hutumika kutibu hali mbali mbali za macho ikiwemo kuvimba inflammation au kuumia,
Pia dawa hii huweza kutumika kuondoa dalili za magonjwa mbali mbali,Ikiwemo dalili kama vile;
- Macho kuwa Mekundu
- Kuvimba
- Kuwasha n.k
Dawa hii ipo kwenye kundi la dawa jamii ya corticosteroids.
Zingitia haya Kabla ya kutumia dawa ya Macho?
– Hakikisha ni Dawa Sahihi kwa ajili ya tatizo lako,
Hivo pata maelekezo ya kina kutoka kwa Wataalam wa afya kwanza kabla ya matumizi
– Angalia muda wa matumizi kwenye dawa yako(Expire date)
– Hakikisha umenawa mikono kwa maji safi na sabuni kabla ya kushika macho na kutumia dawa
– Hakikisha macho,Uso na mwili kwa ujumla ni Safi.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.