Boston, Massachusetts, USA
“Bw Slayman,Mwanamume wa kwanza kupandikizwa figo ya nguruwe iliyobadilishwa vinasaba amefariki miezi miwili baada ya upasuaji huo, hospitali iliyotekeleza utaratibu huo imesema.
Richard “Rick” Slayman, umri 62, alikuwa akiugua ugonjwa wa figo hatua ya mwisho kabla ya kufanyiwa upasuaji huo mnamo mwezi Machi.
“Rick alisema kuwa moja ya sababu zilizomfanya afanyiwe utaratibu huu ni kutoa matumaini kwa maelfu ya watu wanaohitaji upandikizaji kuishi,”
Hospitali kuu ya Massachusetts (MGH) ilisema Jumapili hakuna dalili kwamba kifo chake kilikuwa matokeo ya upandikizaji. Hospitali hiyo ilisema “imehuzunishwa sana” na kifo chake cha ghafla na kutoa rambirambi kwa familia yake.
Bibi apandikizwa figo ya nguruwe pamoja na moyo wa bandia
Bibi mmoja mwenye umri wa miaka 54 amefaulu kupokea upandikizaji wa kwanza wa pamoja wa figo ya nguruwe na pampu ya moyo.
Lisa Pisano, mzaliwa wa New Jersey aliye na ugonjwa wa figo ukiwa katika hatua za mwishoni, pamoja na tatizo la kushindwa kwa moyo kufanya kazi(Heart failure),
alikaa kwa muda pasipo upandikizaji wa moyo na figo kutokana na uhaba wa michango ya viungo vya binadamu na hali sugu za kiafya ambazo zilipunguza uwezekano wake wa kupata matokeo mazuri.
Alisema: “Ninachotaka ni fursa ya kuwa na maisha bora.
“Baada ya kutengwa kwa ajili ya upandikizaji huo nilijifunza sikuwa na muda mwingi uliobaki.
“Madaktari wangu walidhani kunaweza kuwa na nafasi ya kuidhinishwa kupokea figo ya nguruwe iliyohaririwa na jeni, kwa hivyo niliijadili na familia yangu na mume wangu. Amekuwa upande wangu katika kipindi chote cha majaribu haya na anataka niwe bora zaidi.”
Madaktari wa upasuaji wa Afya wa NYU Langone walifanya utaratibu wa ubunifu wa hatua mbili mapema mwezi huu huko New York. Mnamo Aprili 4, walipandikiza kwa upasuaji pampu ya moyo inayoitwa kifaa cha usaidizi cha ventrikali ya kushoto (LVAD) kwenye Pisano.
Kisha Aprili 12, walimfanyia upasuaji wa kupandikiza figo ya nguruwe iliyohaririwa na jeni, ambayo Ilijumuisha tezi ya nguruwe ili kusaidia dhidi ya mwili wake kukataa kiungo cha wanyama.