Mwaka 2023:Watu 8,145,576 walipima Virusi vya UKIMWI (VVU)
Wizara ya Afya imesema kati ya Watu waliopima mwaka 2023, Watu 163,131 walingundulika kuwa na maambukizi ya VVU ukilinganisha na Watu 182,095 mwaka 2022 na Watu 198,042 mwaka 2021 (DHIS2 2023) ambapo waliokuwa wanatumia dawa za kufubaza virusi vya VVU walikuwa 1,663,651 hadi kufkia December 2023 ukilinganisha na Watu 1,612,512 December 2022 na Watu 1,520,589 mwaka 2021.
Taarifa iliyotolewa na Wizara imeeleza yafuatayo ———> “Serikali imeendelea kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI ambapo katika mwaka 2023 jumla ya Watu 8,145,576 walipima Virusi vya UKIMWI (VVU) ukilinganisha na Watu 6,930,758 mwaka 2022 na Watu 6,493,583 mwaka 2021 (Taarifa kutoka mfumo wa DHIS2 2023)”
Katika kuhakikisha kuwa huduma kwa WAVIU zinasogezwa karibu zaidi na jamii, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wa maendeleo imekuwa ikifanya jitihada za makusudi kabisa za kuhakikisha kila kituo cha afya Nchini kinakuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa Waathirika wa UKIMWI.
“Hadi kufikia Desemba 2023 Idadi ya vituo vinavyotoa huduma ya tiba na matunzo vimefikia vituo 7,396 kutoka vituo 7,072 mwaka 2021 na kati ya hivyo CTC kamili ni 3,572 na vituo vya huduma ya Mama na Mtoto (RCHS) vinavyotoa huduma ya kutoa dawa ya kufubaza Virusi vya UKIMWI vipo 3,824” ——— imeeleza Wizara ya Afya.