WAGONJWA WENGI WANASTAHILI HUDUMA ZA KIBINGWA
Na WAF, Ikungi-Singida
Wakati mahitaji ya huduma za afya zinazidi kuongezeka, wagonjwa wengi katika Wilaya ya Ikungi wanaonekana kustahili na kuhitaji huduma za kibingwa.
Hayo yamebainishwa na daktari bingwa wa magonjwa ya ndani Dkt. Antony Abraham ambapo ameeleza kuwa mahitaji ya huduma za kibingwa yanazidi kuongezeka katika jamii, huku akiwa amewaona wagonjwa zaid ya 70
Aidha, Dkt. Abraham ameelezea umuhimu wa kuwa na kampeni endelevu ya madaktari bingwa katika ngazi ya halmashauri na wilaya ili kukabiliana na mahitaji makubwa ya huduma za kibingwa.
Pia, amesema, hali hiyo itasaidia kuhakikisha kila mgonjwa anapata matibabu yanayostahili na yanayolingana na mahitaji yake.
Mwisho.