Kunguni husababisha ugonjwa gani
Kunguni ni wadudu wadogo ambao chakula chao kikubwa ni damu, wadudu hawa huweza kunyonya damu kutoka kwa binadamu au wanyama mbalimbali
Kunguni wanapenda kukaa mazingira ya kujificha kama kwenye godoro,kitanda,chaga za kitanda,kwenye kapeti,kwenye nguo n.k
Kunguni hupenda sana kunyonya damu hasa wakati wa usiku ukiwa umelala
MADHARA AMBAYO MTU HUWEZA KUYAPATA BAADA YA KUNG’ATWA NA KUNGUNI(bedbugs)
– Mtu kupatwa na miwasho mwilini
– Ngozi yako ya mwili kuwa na madoa doa au alama za kung’atwa
– Mtu kukosa usingizi na kutokulala vizuri
– Mtu kuanza kukonda
n.k
Kunguni hupenda sana kukaa kwenye mazingira machafu, na huweza kukung’ata sehemu yoyote ya mwili wako kama vile; usoni,mikononi,mgongoni n.k