Takribani Watu 36,000 wahamishwa chanzo mafuriko makubwa China
Watu wapatao 36,000 wamehamishwa na kupelekwa sehemu salama kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa katika mkoa wa kusini mashariki mwa China wa Fujian.
#PICHA:Sehemu za kuchezea watoto iliyozama kwenye bustani baada ya mvua kubwa kunyesha mkoani Guangdong kusini mwa China.Picha: AFP/Getty Images
Shirika la habari la serikali la Xinhua limeripoti jana kuwa sehemu kubwa ya mkoa huo umeharibiwa na mvua kubwa na kuilazimisha mamlaka kutoa agizo la kuhamisha watu.
Watu 179,800 waliathirika na mvua hiyo kufikia Jumamosi jioni huku mafuriko yakiharibu hekta 12,350 za mavuno sawa na hasara ya dola milioni 225.
Mwishoni mwa wiki, mamlaka ya hali ya hewa iliripoti ongezeko la viwango vya maji katika mito 11 hadi mita 3.65 juu ya kiwango cha tahadhari.
Mamlaka nchini humo imetahadharisha kuwa mvua kubwa inatabiriwa kunyesha katika mikoa kadhaa ikiwemo Zheijan, Fujian, Jiangxi, Hunan, Guangdong na Sichuan.