Bed rest kwa mama mjamzito
Bed rest; hapa tunazungumzia mapumziko ya kitandani kwa mama mjamzito, ambapo kitaalam hushauriwa kulingana na hali yake ya Ujauzito.
Mtoa huduma wako wa afya anaweza kupendekeza kupumzika kitandani ikiwa utatambuliwa una matatizo ya ujauzito kama vile tatizo la kifafa cha mimba(preeclampsia/eclampsia) au tatizo la kutokwa na damu ukeni n.k,
Urefu wa muda ambao uko kwenye mapumziko kitandani(Bed rest) na kile unachoruhusiwa kufanya hutofautiana kulingana na hali yako.
Ikiwa mtoa huduma wako wa afya anapendekeza kupumzika kitandani au kuanza Bed rest inamaanisha kuwa ana wasiwasi kuhusu hali ya afya ambayo inaweza kusababisha matatizo ya ujauzito au leba ya mapema.
Mtoa huduma wako anaweza kukuweka kwenye mapumziko ya kitandani kwa muda wa wiki chache au miezi kadhaa.
Wahudumu wa afya wakati fulani huagiza kupumzika kitandani(Bed rest) wakati wa ujauzito ili kuongeza uwezekano wa mimba yako kukua na kufikia umri sahihi wa kujifungua(term pregnancy).
Kubeba mimba hadi kufikia muda sahihi wa kujifungua kunamaanisha kuwa una ujauzito ambao angalau umefika wiki 37 kabla ya mtoto wako kuzaliwa. Kupumzika kitandani(Bed rest) kunaweza kuhusisha mambo kadhaa kama vile;
- kuzuia shughuli zako,
- kulazwa hospitalini
- au kulala nyumbani.
Mapumziko ya kitandani au Bed rest kwa mama mjamzito huhusisha mambo kadhaa ikiwemo kulala kitandani au kuacha kufanya shughuli n.k,
Kwa mujibu wa “The American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG)” hawashauri ukiwa kwenye Bed rest basi uache kabsa kufanya chochote au kazi bali unashauriwa kupunguza kazi au kupunguza kufanya baadhi ya mambo
(ACOG: They, instead, recommend reducing your usual activities instead of stopping your activities entirely).
Aina za Bed rest kwa mama Mjamzito
Kufanya Bed rest kwa mama mjamzito kunaweza kumaanisha mambo kadhaa, Hakuna ufafanuzi mmoja kuhusu bed rest,
kwa hiyo, zungumza na mtoa huduma wako wa afya kuhusu kile unachoruhusiwa kufanya na ambacho hauruhusiwi kufanya wakati wa mapumziko yako(Bed rest).
Hizi hapa ni aina mbali mbali za Bed rest kwa mama mjamzito;
1. Strict or complete bed rest:
Hii ni aina ya Bed rest kwa mama mjamzito ambapo mama mjamzito haruhisiwi kufanya chochote kabsa,
Hapa mama mjamzito anakuwa kitandani akiwa hospital au nyumbani kwa zaidi ya siku nzima.
Na kwa baadhi ya Visa, Mama mjamzito huletewa bedpan kwa ajili ya kujisaidia,hivo haruhusiwi kutoka kitandani na kwenda chooni.
2. Activity restriction Bed rest:
Hii ni aina ya Bed rest kwa mama mjamzito,ambapo mama mjamzito anatakiwa kupunguza kufanya baadhi ya shughuli na kuepuka kusimama au kutembea kwa muda mrefu,
Hapa mama mjamzito harusiwi kabsa kunyanyua vitu vizito au kutumia ngazi.
3. Modified bed rest:
Aina Hii ya Bed rest kwa mama mjamzito inafanana zaidi na activity restriction bed rest,
Hapa huhusisha mama mjamzito kutumia muda wake mwingi kukaa au kulala chini, na kwa aina hii ya bed rest; mama mjamzito anaruhusiwa kutembea umbali mfupi mara chache kwa siku au kufanya kazi nyepesi za nyumbani.
Kumbuka: Kama umeambiwa uanze Bed rest kama mjamzito; Ni SAWA kumuuliza mtoa huduma wako wa afya kufafanua mapumziko yako ya kitandani(Bed rest) inahusu kufanya vitu gani kulingana na hali yako ili wote muwe kwenye ukurasa mmoja.
Sababu za Bed rest kwa mama mjamzito
Mtoa huduma wako wa afya anaweza kupendekeza kupata mapumziko ya kitandani au Bed rest ili kupunguza uwezekano wa kuzaa mapema/kabla ya wakati au kusaidia kutibu hali ya ujauzito ambayo inaweza kusababisha matatizo kwako au kwa mtoto.
Sababu za kupumzika kitandani au kuanza Bed rest wakati wa ujauzito ni pamoja na;
– Mjamzito Kuwa kwenye hatari ya kupata tatizo la kifafa cha mimba(Preeclampsia/eclampsia)
– Kuvuja Damu Ukeni wakati wa ujauzito(Vaginal bleeding)
Kuvuja damu ukeni wakati wa ujauzito huweza kuashiria matatizo mbali mbali ikiwemo;
- Tatizo la mimba kutoka au kutishia kutoka
- Tatizo la placenta previa (kondo la nyuma/placenta kufunika sehemu au eneo lote la mlango wa kizazi
- Tatizo la placental abruption (kondo la nyuma/placenta kuachia lilipojishikiza kwenye ukuta wa kizazi kabla ya wakati wake).
– Mjamzito kupata uchungu kabla ya wakati wake(Premature labor): Bed rest kwa mama mjamzito inaweza kushauriwa kwa tatizo la mama mjamzito kuanza kupata uchungu wa kujifungua kabla ya wakati wake,
Ikiwa mama mjamzito huanza kupata uchungu kabla ya wiki 37 za Ujauzito, basi moja ya vitu ambavyo atashauriwa kufanya ni pamoja na kupata mapumziko kitandani au kuanza Bed rest mara moja.
– Mjamzito kuwa na tatizo la Mlango wa kizazi kulegea(Incompetent cervix): Hapa tunazungumzia ile hali ya shingo la kizazi(Cervix) kuwa dhaifu sana, na kuanza kufunguka hata kabla ya wakati wake.
Kwa hali hii,Moja ya vitu muhimu sana kwa mama huyu mjamzito ni kuanza Bed rest mara moja.
– Tatizo la Cervical effacement: ambapo mlango wa kizazi au shingo ya kizazi kwa maana ya Cervix kuwa nyembamba sana(Thinning of your cervix).
– Kuwa na mimba ya Watoto zaidi ya mmoja(twins,triplets n.k)
Bed rest kwa mama mjamzito inaweza kushauriwa pia,ikiwa mama mjamzito kabeba mimba ya watoto zaidi ya mmoja.
– Kupata matatizo katika mimba zilizopita(Previous pregnancy complications):
Bed rest kwa mama mjamzito inaweza kushauriwa ikiwa mama mjamzito ana historia ya kupata baadhi ya matatizo kwenye mimba zilizotangulia, matatizo hayo ni pamoja na;
- Ujauzito/Mimba kutoka zenyewe,
- Kuzaa mtoto aliyekufa(stillbirth)
- Au kujifungua mapema/kabla ya wakati(premature birth).
– Kupata tatizo la mtoto kutokukua au kudumaa akiwa bado tumboni(Intrauterine growth restriction),n.k
KUMBUKA: ni muhimu kujua ni kwanini umeambiwa uanze Bed rest ukiwa mjamzito, na pia uelezewe ni aina gani ya bed rest unatakiwa kuifuata kulingana na hali yako, ikiwa na maana ujue vitu gani unapaswa kufanya na vipi hurusiwi kabsa kufanya kulingana na Hali yako.
Faida za Bed rest kwa mama mjamzito
Zipo faida nyingi za Bed rest kwa mama mjamzito ikiwemo;
✓ Kusaidia kuzuia matatizo mbali mbali kipindi cha Ujauzito(pregnancy complications) ikiwemo;
- Ujauzito/Mimba kutoka zenyewe,
- Kuzaa mtoto aliyekufa(stillbirth)
- Mama mwenyewe kupoteza maisha
- Au kujifungua mapema/kabla ya wakati(premature birth).
✓ Kusaidia katika Utunzaji wa ujauzito na kuzuia ujauzito kutoka au kuzuia mwanamke kujifungua kabla ya wakati wake(premature birth)
✓ Kusaidia kupunguza Stress za Ujauzito
✓ Kusaidia kupunguza mgandamizo au presha kwenye Shingo ya kizazi(Cervix)
✓ Kusaidia kupunguza shinikizo la damu(Blood pressure)
✓ Kusaidia kondo la nyuma au placenta kufanya kazi vizuri zaidi, hii husaidia katika usafirishaji mzuri wa virutubisho pamoja na hewa safi ya oxygen kwenda kwa mtoto.n.k
Nini naruhusiwa kufanya na nini siruhusiwi kufanya wakati wa Bed Rest kama mama mjamzito
Kumbuka tulipotoka, tumeelezea aina mbali mbali za Bed rest kwa mama mjamzito, ambazo aina hizi hutegemea kwa asilimia 100% hali ya mama mjamzito kwa wakati huo.
Hivo nini unaruhusiwa kufanya na nini huruhusiwi kufanya inategemea na hali yako ya Ujauzito kwa kipindi hicho;
Mfano wa vitu ambavyo huweza kuruhusiwa kulingana na hali yako ukiwa kwenye bed rest;
- Kutembea wakati unaenda bafuni au chooni
- Kukaa na kulala
- Kutembea umbali mfupi ndani ya nyumba au nje kwa muda usiozidi dakika 20
- Kusimama kwa muda wa dakika chache
- Kufanya kazi zinazohusisha kukaa kwenye kiti
- Kufanya Zoezi la kupanda ngazi kwa kiasi(mara moja kwa siku)
- Kuoga mara moja kwa siku n.k
Mfano wa vitu ambavyo vinaweza visiruhusiwe kulingana na hali yako ukiwa kwenye bed rest;
- Kufanya Shughuli yoyote ambayo huchukua zaidi ya dakika 30 ukiwa umesimama au kutembea kwa wakati mmoja.
- Kunyanyua Vitu vizito sana
- Kuweka kitu chochote Ukeni
- Kufanya mapenzi kwa aina yoyote ile n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.