FAIDA YA TIKITI MAJI KWA MAMA MJAMZITO
Tunda hili la Tikiti maji ni miongoni mwa matunda yenye kiwango kikubwa cha Maji, pamoja na nutrients nyingine muhimu mwilini kama vile Proteins,Vitamins,Minerals, pamoja na uwepo wa Fibers.
Hizi hapa Chini ni Baadhi ya Faida za tunda la Tikiti Maji kwa Mama Mjamzito
- Tunda la tikiti Maji husaidia kuongeza kiwango cha Maji mwilini ambayo ni muhimu sana kwa mama mjamzito kutokana na kuongezeka kwa mahitaji yake mwilini,
- Tunda la tikiti maji huweza kusaidia kupunguza uwezekano wa kutokea kwa shida ya Kifafa cha Mimba kwa mama mjamzito,
Hii ni kutokana na baadhi ya tafti,japo kuna umuhimu zaidi wa kupafanya Research juu ya hili,
Zipo tafiti zinasema kwamba, uwepo wa kiwango kikubwa cha Compound ya LYCOPENE ambayo hutoa pigment za rangi nyekundu kwa matunda kama tikitimaji,Nyanya pamoja na matunda mengine yenye rangi nyekundu husaidia pia kuzuia hatari ya kutokea kwa kifafa cha Mimba,
Tafiti hyo inasema kwamba,4mg za Lycopene kwa siku au asilimia 60% ya Lycopene ndani ya Kikombe kimoja(152mg) cha tikiti maji huweza kusaidia kupunguza kutokea kwa kifafa cha mimba au Preeclampsia mpaka kwa kiwango cha asilimia 50%, NOTE:Tafiti zaidi huhutajika katika hili
- Pia tunda la tikiti maji huweza kupunguza complications mbali mbali ambazo huweza kutokea kipindi cha ujauzito,
kuongeza Blood volume kutokana na uwepo wa kiwango kizuri cha maji,kuongeza maji ya uzazi au amniotic fluid n.k
- Tikiti maji hupunguza hatari za kutokea kwa tatizo la mama mjamzito kupata choo kigumu pamoja na matatizo mengine kama vile,michubuko sehemu ya haja kubwa,maumivu wakati wa kujisaidia,tatizo la bawasiri n.k
- Pia kutokana na uwepo wa kiwango kikubwa cha maji kwenye tunda hili la tikiti maji,basi huweza kusaidia pia kupunguza maambukizi kwenye njia ya mkojo au UTI n.k
- Tunda la tikiti maji lina antioxidants ambayo pia ni muhimu kuzuia madhara mbali mbali
-Tunda la tikiti maji huweza kusaidia pia mtu kupata usingizi mzuri n.k
KUMBUKA; TUNDA LA TIKITI MAJI ni Salama kwa Mama mjamzito ila matumizi ya kiwango kikubwa cha tunda hili husababisha kuongezeka kwa kiwango cha Carbs na kupungua kwa FIBER,combination hii huweza kusababisha kiwango cha Sukari kwenye damu kuongezeka
• Hivo kwa mama mjamzito mwenye historia ya kupata kisukari wakati wa ujauzito yaani Gestational Diabetes au mwenye viashiria vya kupatwa na kisukari cha Mimba anashauriwa kuepuka matumizi ya kiwango kikubwa cha tunda la Tikitimaji
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.