SABABU ZA MTU KUWA NA VIDONDA MDOMONI
Baadhi ya watu hupatwa na tatizo la kuwa na vidonda mdomoni,na vidonda hivo huweza kuwa maeneo tofauti ya mdomo kama vile kwenye kuta za juu ya mdomo,pembeni,chini ya ulimi,kwenye ulimi au nje kwenye lips za mdomo,
Je hali hii huweza kusababishwa na nini?,zipo baadhi ya sababu mbali mbali ambazo tumezichambua hapa,sababu hizi huweza kuwa chanzo cha mtu kuwa na vidonda mdomoni
SABABU ZA MTU KUWA NA VIDONDA MDOMONI NI PAMOJA NA;
- Mtu kula chakula mara kwa mara ambacho kimekosa virutubisho muhimu sana kama vile; vitamin B12,Madini ya Zinc,Foleti pamoja na madini ya Chuma
- Majeraha yanayotokana na mtu kupiga mswaki,kujing'ata,kutumia grili ya meno n.k
- Kuunguzwa mdomoni na vitu vya moto kama vile chai pamoja na vinywaji vingine vya moto sana
- Matumizi ya dawa mbali mbali pamoja na vimiminika vyenye Sodium sulphate ndani yake wakati wa kusafisha meno
- Magonjwa mbali mbali kama vile; maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI,Fangasi,Seliak n.k
- Tatizo la allergy au mzio,homa za usiku n.k
- Tatizo la saratani ya kwenye kinywa(mdomoni),ulimi au saratani ya damu
- Mtu kupatwa na magonjwa mbali mbali ya ngozi,ambapo mtu huweza kuwa na vidonda kwenye ngozi ya ndani ya mdomo,nje ya mdomo,pamoja na maeneo mengine mwilini
KUMBUKA; Kuna wakati vidonda hivi vya mdomoni huweza kuambatana na miwasho mikali au mtu kupata shida ya kumeza kitu pamoja na maumivu wakati wa umezaji wa kitu chochote
VIPIMO VYA TATIZO HILI
Ili kugungua chanzo cha tatizo la vidonda mdomoni;
- Mgonjwa huweza kuulizwa kuhusu historia ya ugonjwa ulivyoanza(patient history taking)
- Kuchukua sample ya damu na kuchunguza vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile;virusi,bacteria au fangasi n.k
MATIBABU YA VIDONDA MDOMONI
Tatizo hili hutibika kulingana na chanzo husika,kama nilivyokwisha kuelezea baadhi ya sababu zinazochangia uwepo wa tatizo la vidonda mdomoni,
Hivo mtu mwenye shida hii lazima akutane kwanza na wataalam wa afya,ndipo apewe maelekezo kamili kuhusu vipimo pamoja na matibabu
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.