Je,Mkojo kutoa harufu ya dawa unazotumia ni tatizo?
Mkojo kutoa harufu ya dawa unazotumia; Watu wengi wamekuwa wakisema au kulalamika,dawa ninazotumia nasikia harufu yake kwenye Mkojo wakati nakojoa,
Je,ni kawaida au ni tatizo kusikia harufu ya dawa unazokunywa kwenye mkojo? Soma hapa kufahamu;
Hapana sio tatizo,
Dawa; Baadhi ya dawa kama vile dawa jamii ya antibiotics zinaweza kufanya mkojo wako kunuka au kuwa na harufu ile ile ya dawa ulizokunywa.
Baadhi ya viuavijasumu(antibiotics) hutengenezwa kwa kutumia mold au vimelea vya fangasi hali ambayo huweza kufanya mkojo wako kuwa na harufu ya chachu(Smell yeasty). Kunywa maji mengi siku nzima kunaweza kusaidia kupunguza harufu hizi na kuweka mkojo wako Safi.
Dawa kama vile penicillin pia zinaweza kuathiri jinsi mkojo unavyotoa harufu, kwani baadhi ya viambato vinavyoingia kwenye dawa hii hutokana na mould ambayo inaweza kuupa mkojo harufu inayofanana na chachu au tunaita yeasty smell.
Hata hivyo, hali hii ya Mkojo kutoa harufu ya dawa unazokunywa haina madhara kabisa, Ingawa haitakiwi kuendelea baada ya kumaliza dawa. Ikiwa bado mkojo unatoa harufu ya dawa ulizotumia wakati ulishamaliza dawa muda hakikisha unafanya uchunguzi zaidi.
Dawa zenye salfa zinaweza kutoa uvundo au harufu pia kwenye mkojo wako. Hiyo ni pamoja na antibiotics zenye sulphur(sulfonamide antibiotics) ambazo hutumika sana kutibu UTI na maambukizi mengine.
Dawa za kisukari pamoja na arthritis(baridi yabisi) pia zinaweza kuathiri jinsi mkojo wako unavyotoa harufu. Ikiwa harufu mbaya inakusumbua sana kiasi kwamba inaleta athari zingine waambie wataalam wa afya kuhusu hilo. Wanaweza kutaka kuhakikisha kuwa hakuna kitu kingine kinachosababisha harufu hiyo.
Ina maana gani Mkojo kutoa harufu ya dawa unazotumia?
Unaposikia kwamba mkojo unatoa harufu ya dawa unazotumia, mara nyingi hili linaweza kuwa dalili ya kwamba mwili wako unatoa nje baadhi ya viambato ambavyo vimefyonzwa kutoka kwenye dawa hizo.
Kwa mfano, baadhi ya dawa zinaweza kubadilishwa kikamilifu au kwa sehemu katika mwili wako, na viambato hivyo vinaweza kutolewa nje ya mwili kupitia mkojo.
Kumbuka kwamba harufu ya mkojo inaweza kubadilika kwa sababu nyingi, ikiwa ni pamoja na;
- kiasi cha maji mwilini,
- vyakula unavyokula,
- na hali yako ya kiafya kwa ujumla.
Soma Zaidi hapa;Sababu zingine za Mkojo kutoa harufu kali.
Hata hivyo, ikiwa unatumia dawa ambayo inatoa harufu maalum kwenye mkojo, ni muhimu kuzingatia hilo na kuwa tayari kuelezea hilo kwa daktari wako au mtaalamu wa afya ikiwa ni sehemu ya utathmini wa afya yako.
Kwa upande mwingine, daima ni muhimu kuchukua dawa kama ilivyoagizwa na daktari wako na kufuata maagizo yake. Ikiwa una wasiwasi kuhusu athari yoyote au dalili zinazoonekana wakati wa kutumia dawa, ni muhimu kuwasiliana na daktari wako mara moja.
Kwa kuongezea; ni muhimu pia kuhakikisha unashirikiana kikamilifu na wataalam wa afya na kueleza kuhusu historia yako ya matibabu na dawa unazotumia ili kuhakikisha kuwa unapokea huduma bora na salama zaidi.