TATIZO LA TUNDU KWENYE MOYO(VENTRICULAR AND ATRIAL SEPTAL DEFECT)CHANZO,DALILI NA TIBA
A. VENTRICULAR SEPTAL DEFECT
- Hili ni tatizo la uwepo wa tundu kwenye moyo ambalo hutokea kwenye kuta(septum)za chemba ya chini kwenye moyo yaani Ventricles na kusababisha damu kuflow kutoka upande wa kushoto wa moyo kwenda upande wa kulia.
Dalili za tatizo hili huanza kuonekana kwenye siku za mwanzo kabsa,au ndani ya wiki au miezi kadhaa baada ya mtoto kuzaliwa
DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;
- Mtoto kushindwa kunyonya vizuri au kula
- Shida ya kupumua kwa haraka zaidi au kukosa pumzi
- Mwili kuchoka zaidi n.k
CHANZO CHA TATIZO HILI
Tatizo hili la tundu kwenye moyo hutokea wakati wa uumbaji wa moyo wa mtoto akiwa tumboni,hapo ndyo hutokea matatizo au defects, mpaka sasa hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo inahusishwa na tatizo hili ila kuna baadhi ya sababu tu ambazo huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata shida hii kama vile;
• Matatizo kwenye vinasaba,
• Hali ya kimazingira
• Pamoja na matatizo mengine kama vile down syndrome n.k
MADHARA YA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;
- Moyo kushindwa kufanya kazi au heart failure
- Kupatwa na presha kwenye mapafu yaani Pulmonary hypertension
- Kupatwa na shida ya endocarditis
- Shida ya mapigo ya moyo kutokueleweka, shida kwenye valve za kwenye moyo n.k
VIPIMO AMBAVYO HUWEZA KUFANYIKA NI PAMOJA NA
1. kipimo cha Echocardiogram maarufu kama ECHO
2. kipomo cha Electrocardiogram (ECG)
3. chest X-ray
4. Cardiac catheterization
5. Pulse oximetry
6. MRI
7. CT Scan n.k
MATIBABU YA TATIZO HILI
Kama tundu ni dogo sana litafunga lenyewe hivo doctor wa mtoto huyo huweka uangalizi tu wakaribu na kudhibiti dalili zozote zinazojitokeza mpaka tundu lifunge lenyewe,
Ila kama tundu ni kubwa zaidi,matibabu kwa njia ya upasuaji lazima kufanyika na kuziba tundu hilo
B. ATRIAL SEPTAL DEFECT(ASD)
- Hili ni tatizo la uwepo wa tundu kwenye moyo ambalo hutokea kwenye kuta(septum)za chemba ya juu kwenye moyo yaani Atricles/Atrium
DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;
- Mtu kukosa pumzi hasa wakati anafanya mazoezi
- Mwili kuchoka kupita kawaida
- Mtu kupata shida ya kuvimba miguu,mikono au tumbo
- Mapigo ya moyo kwenda mbio au kubadilika na moyo kudunda isivyo kawaida
- Mtu kupatwa na tatizo la Stroke
- Kusikika kwa sauti zisizozakawaida kwenye kifaa cha Stethoscope,nasauti hizo hujulikana kama Heart murmur n.k
CHANZO CHA TATIZO HILI
Tatizo hili la tundu kwenye moyo hutokea wakati wa uumbaji wa moyo wa mtoto akiwa tumboni,hapo ndyo hutokea matatizo au defects, mpaka sasa hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo inahusishwa na tatizo hili ila kuna baadhi ya sababu tu ambazo huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata shida hii kama vile;
1. Uwepo wa maambukizi ya Rubella yaani Rubella Infection
2. Matumizi ya baadhi ya Dawa ambazo haziruhusiwi wakati wa ujauzito
3. Matumizi ya pombe na Sigara au tumbaku(Tobacco) wakati wa ujauzito
4. Mama mjamzito kusumbuliwa na matatizo mengine kama vile kisukari yaani Diabetes, Tatizo la Lupus n.k
MATIBABU YA TATIZO HILI
Tundu hili huweza kuziba lenyewe wakati bado mtoto akiwa ni mdogo, ila kama tatizo litaendelea bila kupona ndipo wataalam wa afya huweza kufanya upasuaji na kuziba tundu hili pamoja na matumizi ya dawa mbali mbali kama vile;
Dawa za kusaidia moyo uendelee kufanya kazi vizuri bila shida, Dawa za kuzuia hatari ya damu kuganda yaani Anticoagulants n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.