Jinsi ya kutambua matatizo ya kiafya kupitia kucha
Ni muhimu kuzingatia mabadiliko ya rangi ya kucha kwani yanaelezea hali ya afya yako.
Kutunza kucha zako ni zaidi ya kwenda kwenye saluni za urembo wa kucha. Sehemu hii ya mwili, inaweza kuonyesha matatizo mbalimbali ya afya.
Ni muhimu kuzingatia mabadiliko ya rangi, kwenye kucha zako na vipengele vingine vinavyotumika kama tahadhari kwa magonjwa mengi. Ili dalili zinapotokea, iwe rahisi kutafuta msaada kwa wataalam wa afya mapema ambao watatathmini kwa kina na kufanya vipimo kama vile vya damu na vinginevyo kulingana na hali yako.
Endapo kitu kikubwa kikishukiwa, mtaalamu anaweza kuagiza seli au tishu kuondolewa kwa uchunguzi zaidi.
Kuna magonjwa ambayo yanachukua muda kujulikana, yanayoathiri sehemu moja au zaidi za mwili, ambayo hutokea kwenye miguu na mikono,
Mara nyingi Matatizo hayo husababishwa na figo, ngozi, ini, lishe, na hali ambayo mfumo wa kinga ya mwili hushambulia seli zenye afya.
Wakati mwingine yali ya kucha zako kubadilika haitokani na tatizo kubwa la kiafya bali masuala ya Urembo hasa kwa Wanawake.
Pia kitu kingine ni utunzaji wa kucha zako;
“Kucha za miguuni hazitunzwi sana na wakati mwingine zinakabiliwa na matatizo zaidi. Ukucha, kwa mfano, unaweza kuwa njano na mzito,” anasema ValĂ©ria Zanela Franzon, daktari wa ngozi na profesa wa Tiba katika Chuo Kikuu cha Katoliki huko Paraná (Pucpr).
Jinsi ya kutambua matatizo ya kiafya kupitia kucha
Zifuatazo ni ishara kadhaa ambazo zinaweza kuonyesha matatizo ya kiafya na zinastahili kuzingatiwa:
1.Kucha nyeupe
• Rangi ya kucha lazima izingatiwe wakati mtu anapoona mabadiliko yasiyo ya kawaida. Kwa mfano; kucha kuwa na rangi nyeupe pamoja na kivuli chepesi kinaweza kuashiria mtu ana ugonjwa wa mycosis unaosababishwa na kuambukizwa na vimelea vya magonjwa.
• Pia Psoriasis, ugonjwa wa ngozi unaosababisha vipele ambavyo huwasha,ngozi kuwa na mabaka mabaka, magamba, mara nyingi kwenye magoti, viwiko, shina na ngozi ya kichwa, na pneumonia au homa ya mapafu na hata moyo kushindwa kufanya kazi vizuri.
• Ukosefu wa baadhi ya virutubisho, utapiamlo na kutopata vyakula vya protini vya kutosha pia husababisha hali kama hii(picha).
• “Kuwa na kucha nyeupe kunaweza pia kuonyesha upungufu wa damu.
Upungufu huu Husababishwa na ukosefu wa madini ya chuma na unaweza kufanya ukucha uwe na umbo la kijiko na kukunjamana,” asema Juliana Piquet, daktari wa ngozi na mshiriki wa Jumuiya ya Madaktari ya Ngozi ya Brazil na Jumuiya ya Amerika kwa Tiba ya Laser na Upasuaji.
• Pia kuna hali inayojulikana kama Leukonychia.
leukonychia, ni madoa meupe kwenye kucha kwa kawaida si ishara ya kutisha, lakini wakati mwingine inaweza kufichua matatizo makubwa ya kiafya.
NB: Unashauriwa kufanya vipimo mbalimbali ili kufahamu mabadiliko yako ya kucha yanaashiria tatizo gani linalokusumbua.
2. Kucha ya njano
Rangi hii inaweza kuwa na sifa ya urithi wa maumbile au kwa sababu ya kuzeeka,
Inaweza pia kutokana na rangi inayosababishwa na mashambulizi ya fungasi kwenye kucha
Katika hali mbaya zaidi, pia inaonyesha hali kama vile psoriasis, Virusi Vya Ukimwi, na ugonjwa wa figo.
3. Kucha zenye mabaka meupe
Mabaka haya yanajulikana kama “pitting” dots na yanaweza kuonekana kwenye kucha.
Yanahusishwa na ugonjwa wa ngozi unaojulikana kama atopic dermatitis -hali ambayo husababisha ngozi kuwa kavu, kuwasha na kuvimba na hali nyingine za ngozi na nywele.
Ni kawaida kwa watoto wadogo, lakini inaweza kutokea katika umri wowote.
4. Kucha kuwa na rangi ya bluu
Ingawa ni nadra kutokea, rangi hii inaweza kutokana na matumizi ya dawa maalum. Mojawapo ya dawa ni zile zinazotibu chunusi na dawa za malaria ambazo hutumiwa kutibu malaria.
Wakati hali hii inapojitokeza, daktari lazima atathmini ikiwa kuna haja ya kusimamisha dawa fulani na kuendelea na aina mpya ya matibabu.
“Inazingatiwa ikiwa kucha ndio udhihirisho pekee na athari ya pili inayokubalika”, anaongeza ValĂ©ria Zanela Franzon, kutoka P ucpr.
Je,vipi kwa upande wa upungufu wa damu?
5. Kucha yenye maambukizi ya mara kwa mara ya vimelea
Ugonjwa wa mycosis unasababishwa na maambukizi ya vimelea na unaweza kutokea tena wakati matibabu yanapositishwa.
Wakati ufuatiliaji haufanyiki vizuri, vimelea vinaweza kutokea na kushambulia kucha mara kwa mara.
Tatizo linaathiri zaidi kucha za miguuni na linapaswa kutibiwa hadi miezi sita,
Likitokea Katika mikono inashauriwa kutibu kwa muda wa miezi mitatu hadi minne.
Muathiriwa anapaswa kuzingatia wakati unaofaa wa kila dawa na kufuata kwa makini ushauri wa daktari hadi matibabu yatakapokamilika.
6. Kucha yenye mistari
Mistari hii inajulikana kama mistari ya Beau, inafanana na mistari ya horizotal na inaweza kuonekana baada ya homa kali au matibabu maalum.
Wakati kiwewe kinatokea katika eneo hilo, ni kawaida kwa mistari kuundwa mahali hapo, na kuacha ukucha ukiwa na makunyanzi zaidi.
Wakati mistari unapokuwa giza na kuonekana kwenye kidole kimoja tu, inaashiria hali inayofahamika kama melanoma, ambayo ni saratani ya ngozi.
KUMBUKA: Unashauriwa kufanya vipimo mbalimbali ili kufahamu mabadiliko yako ya kucha yanaashiria tatizo gani linalokusumbua.