FAHAMU:Parachichi Linaweza kusaidia afya ya moyo, Parachichi lina mafuta mengi asilia yanayoweza kukulinda dhidi ya magonjwa ya moyo.
1.Parachichi linatajwa kama tunda lenye virutubisho vingi, Parachichi ni chanzo bora cha mafuta na lina vitamini E, na ni chanzo kizuri cha virutubishi. Pia hutoa nyuzinyuzi nyingi zaidi kuliko matunda mengine na yana idadi ya madini muhimu ikiwa ni pamoja na chuma, shaba na potasiamu.
2. Parachichi Linaweza kusaidia afya ya moyo, Parachichi lina mafuta mengi huku asilimia 60 ya haya yakiwa ni mafuta asili, ambayo utafiti unapendekeza kuwa husaidia kulinda dhidi ya magonjwa ya moyo na kupunguza shinikizo la damu. Pia ni chanzo bora cha potasiamu, virutubishi na nyuzi, ambavyo vyote hunufaisha moyo na mfumo wa moyo na mishipa.
3.Inaweza kusaidia kupunguza lehemu inayotolewa na parachichi pamoja na asidi ya mafuta ya mbegu. Mafuta haya ambayo hayajajazwa hupendekezwa kama sehemu ya lishe bora ili kusaidia kudhibiti lehemu(cholesterol).
4.Inaweza kusaidia kudhibiti hamu ya kula, hakuna shaka kwamba maudhui ya kalori ya parachichi ni kubwa zaidi kuliko matunda na mboga nyingine.Hata hivyo, uchunguzi wa kuvutia umeonesha kuwa mafuta ya parachichi husababisha hisia za shibe ambayo husaidia kudhibiti hamu ya kula.
5.Inaweza kusaidia kuweka macho yenye afya Kando na faida zilizotajwa hapo juu, parachichi ni chanzo kikubwa cha vitamini E ya kinga, pamoja kusaidia macho yenye afya.