Jinsi ya Kupunguza Hatari ya Kupata Kisukari
Kisukari ni ugonjwa hatari ambao unaweza kusababisha madhara makubwa kwa afya yako. Kwa bahati mbaya, idadi ya watu wanaougua kisukari inaongezeka kila mwaka, hivyo ni muhimu kuchukua hatua za kuzuia ugonjwa huu mapema kabla ya kujitokeza.
Pata picha tu Kwa Mujibu wa Takwimu za Shirika la afya Duniani(WHO)
Idadi ya watu wenye Ugonjwa wa Kisukari(diabetes) Duniani iliongezeka kutoka Million108 mwaka1980 mpaka kufikia Watu million 422 kwa mwaka 2014, Je kama Idadi inaongezeka kila mwaka leo hali Ipoje?
Pia ugonjwa huu wa Kisukari ni chanzo kikubwa cha matatizo mengine kama vile;
- Upofu wa macho(blindness),
- Tatizo la Figo kushindwa kufanya kazi(kidney failure),
- Shambulio la moyo(heart attacks),
- Tatizo la kiharusi(stroke)
- Pamoja na Tatizo la watu Kukatwa MIGUU
• Soma zaidi hapa,Dalili za Ugonjwa wa Kisukari
Kuna hatua kadhaa za kufuata ili kupunguza hatari ya kupata kisukari, na makala hii itakusaidia kujifunza jinsi ya kufanya hivyo.
1.Kula vyakula sahihi
Vyakula vyenye kiwango cha juu cha sukari, wanga, na mafuta yasiyofaa ni hatari kwa afya yako na vinaweza kuongeza hatari ya kupata kisukari.
Kwa hiyo, ni muhimu kuzingatia ulaji wa vyakula sahihi, kama vile matunda, mboga mboga za majani, protini, na wanga unaochujwa.
2. Fanya Mazoezi ya mara kwa mara
Mazoezi ya mara kwa mara yanasaidia kupunguza hatari ya kupata kisukari,
Jaribu kufanya mazoezi kwa angalau dakika 30 kwa siku, angalau siku tano kwa wiki.
Mfano wa mazoezi haya ni pamoja na
- Mazoezi ya kutembea,
- kukimbia,
- kuogelea,
- Kuendesha baiskeli,
- Pamoja na yoga.
3. Punguza Unene wa mwili
Unene wa mwili ni hatari kwa afya yako na inaweza kuongeza hatari ya kupata kisukari. Kwa hiyo, ni muhimu kupunguza uzito wako kwa kupitia lishe bora na mazoezi ya mara kwa mara.
4. Tumia Maji ya kutosha
Unywaji wa maji wa kutosha ni muhimu kwa afya yako na inaweza kusaidia kupunguza hatari ya kupata kisukari. Jaribu kunywa angalau lita 2.5 ya maji kwa siku.
5. Punguza Matumizi ya Pombe
Hitimisho:
Kupunguza hatari ya kupata kisukari ni muhimu kwa afya yako na inaweza kusaidia kuepuka madhara makubwa ya ugonjwa huo.
Kwa kuzingatia lishe bora, mazoezi ya mara kwa mara, unywaji wa maji wa kutosha, na kupunguza matumizi ya pombe, unaweza kupunguza hatari kwako ya kupata kisukari.
Ni muhimu kufuata hatua hizi kama njia ya kudumu ili kuhakikisha afya yako na kuepuka hatari ya kupata kisukari.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.