Zaidi ya wanawake 100 wahukumiwa kifungo kwa kuwatuma watoto wao kuwa omba omba.
Mahakama nchini Uganda imewahukumu zaidi ya wanawake 100 kifungo cha mwezi mmoja kila mmoja baada ya kukiri kuwatuma watoto wao kuwa omba omba katika mji mkuu wa Kampala.
Mahakama hiyo pia imepiga marufuku wanawake hao kurejea mjini na kuamuru warudishwe kijijini kwao, gazeti la kibinafsi la Daily Monitor liliripoti.
Hata hivyo wanawake hao waliomba kuhurumiwa, huku wengine wakisema ni wajane na wengine ni mama wasio na wenza, gazeti la serikali la New Vision liliripoti.
Je, hatua ya namna hiyo itasaidia kupunguza watoto ombaomba mtaani?