Uingereza yaongoza matumizi ya Pombe kwa Watoto.
Theluthi moja ya watoto wenye umri wa miaka 11 na zaidi ya nusu ya watoto wa umri wa miaka 13 nchini Uingereza wamekunywa pombe, na kuifanya nchi hiyo kuongoza kati ya nchi 44 zilizochunguzwa katika ripoti ya wataalam wa afya duniani.
Ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ilisema unywaji wa pombe, ambao unaweza kuharibu ubongo wa watoto, kumefanywa kuwa jambo la kawaida.
Wasichana waligundulika kuwa na uwezekano zaidi kuliko wavulana kunywa na kulewa wakiwa na umri wa miaka 15 huko Uingereza.