Vipele kwenye uume
Ni dalili inayotokea sana kwa wanaume, licha ya kuweza sababishwa na magonjwa ya zinaa, mara nyingi vipele hivi husababishwa na sababu za kawaida.
Uume ni sehemu muhimu ya mwili kwa kila mwanaume ndio maana mabadiliko yoyote yakitokea huwa yanaleta hofu na wasiwasi. Licha ya kuweza kutia wasiwasi, si wakati wote kwamba vipele au uvimbe kwenye uume hutokana na sababu za hatari. Makala hii imeelezea baadhi ya visababishi vikuu vya uvimbe na vipele kwenye uume. Makala hii imeandikwa kwa lengo la kuelimisha tu, ili kufahamu zaidi kuhusu kisababishi halisi cha vipele kwenye uume wako, unashauriwa kuwasiliana na daktari.
Visababishi
Visababishi vikuu vya vipele na uvimbe kwenye uume ni;
Mole
Ni vijivimbe visivyo vya hatari vinavyotokana na ngozi kuzalisha pigmenti nyingi za rangi nyeusi kwenye eneo digo. Uvimbe wa aina hii unaweza kuonekana sehemu yoyote ule ya mwili ikiwa pamoja na kwenye uume. Kwa wastani watu huwa na takribani mole 10 hadi 40 sehemu mbalimbali za mwili
Picha chini inaonyesha aina za mole
Wakati gani wa kuonana na daktari?
Mara nyingi uvimbe wa mole huwa hauna hatari, hata hivyo endapo unabadilika umbile, rangi, kuwa na umbile lisiloeleweka na kubadilika muundo, wasiliana na daktari haraka kwa uchunguzi ili kuchunguzwa kama ni saratani au la.
Maoteo ya vinyweleo ndani ya ngozi
Hutokea kama kipande cha nywele iliyokatwa kimezuliwa kutoka nje ya ngozi kutokana na kuziba kwa vishimo vya vinyweleo na hivyo kutengeneza uvimbe chini ya ngozi. Uvimbe huu unaweza kuleta dalili ya kuwasha au maumivu na wakati mwingine kutengeneza usaha au majimaji. Mara nyingi hutokea mara baada ya kunyoa nyweke za maeneo hayo hivi karibuni.
Ili kuondoa vipele hivi, vinyweleo vilivyootea chini ya ngozi vinapaswa kunasuliwa au kutolewa na mtaalamu wa afya.
Maambukizi ya bakteria au fangasi kwenye kinyweleo kilichojificha chini ya ngozi hupelekea ugonjwa wa ngozi wenye jina la folikilaitiz.
Angalia picha inayofuata kwa maelezo zaidi.
Kifuko maji
Ni uvimbe usio wa hatari wenye ukuta wa epithelia na maji ndani yake pasipo kuwa na kitundu mtoleo cha maji hayo. Huweza kutokea sehemu yoyote ya mwili ikiwa pamoja na uume.
Kifuko maji mara nyingi hufanana na rangi ya ngozi na hakina maumivu na kutobadilia mwonekano licha ya kuweza kuwa kubwa.
Fodisi spoti
Fodisi spoti ni kiuvimbe kidogo chenye rangi nyeupe kinachoweza kuonekana kwenye ncha ya ulimu au ndani yam domo pamoja na meneo ya siri kama kwenye uume.
Viuvimbe hivi ni aina ya tezi ndogo za sebaceous zisizofanana na tezi za kawaida na huwa haziambatani maeneo yenye vinyweleo. Huhitaji matibabu kwenye aina hii ya vipele.
Angalia picha chini kwa maelezo zaidi.
Pearly penile papule
Ni vipele laini vinavyovyozunguka kwenye shingo ya uume na huzunguka uume wote kwenye mstari mmoja wa duara au mistari miwili. Vipele hivi huchukuliwa kuwa vya kawaida na havileti dalili totote wala kuhitaji matibabu.
Angiokeratoma
Ni vipele vidogo vinavyotokea katika mkusanyiko kwenye maeneo ambapo mishipa ya damu upo karibu na usawa wa ngozi au karibu na mshipa wa damu uliotanuka.
Angiokeratoma huweza kuwa na umbile lisiloeleweka na kuogezeka ukubwa. Huweza kumaanisha kuwa na ugonjwa wa mishipa ya damu kama vile shinikizo la juu la damu au varikosili. Unapaswa kuwasiliana na daktari kama ukipatwa na tatizo kama hili.
Ugonjwa wa Pironiaz
Ugonjwa wa Pironiaz hutokana na tishu za makovu za faibrazi kutengenezwa kwenye uume na kufanya ujikunje na kuwa na mwonekano usioeleweka au kutengeneza uvimbe.Uume unaweza kupata maumivu wakati wa kusimama na kupelekea pia madhaifu ya kusimamisha uume.
Ugonjwa Pironiaz huongezeka muda unavyokwenda, unapaswa kuwasiliana na daktari mara moja upatwapo na dalili hii.
Limfosil
Limfosil ni uvimbe mgumu unaoweza kuonekana kwenye uume baada ya kufanya ngono au punyeto. Hutokea kufuatiwa kuziba kwa muda kwa moja ya mshipa limfu. Mara nyingi limfosili huisha haraka bila matibabu yoyote.
Molluscum contagiosum
Ni ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na uambukizo wa gozi na virusi. Huzalisha vipele vidogo, laini, vinavyong’aa na kujazwa na nta ndani. Huweza kuonekana sehemu yoyote ya mwili na hutokea sana kwa watoto
Herpes ya sehemu za siri
Vipele au uvimbe wa herpes husabaishwa na uambukizo wa sehemu za siri na kirusi herpes simplex 1 au 2 (HSV-1 au HSV-2).
Sifa zingine
Vipele hivi huwa vimejazwa na maji na huwa na maumivu au kuwasha. Vipele hivi huhitaji matibabu ya dawa za virusi na za maumivu ili kudhibiti dalili.
Sunzua
Sunzua au warts za shemu za siri husababishwa na uambukizo wa kirusi human papilloma (HPV).
Sifa zingine
Huzalisha kipele au uvimbe usio na maumivu maeneo ya kuzunguka uume au uke na njia ya haja kubwa.
Huweza kuwa laini, rangi ya kijivu nyeupe, pinki- nyeupe au kahawia na huweza kuwa mmoja au kwenye kundi na wakati mwingine huchanua na kuwa na umbile kama la uyoga uliosambaa.
Dawa mbalimbali zinaweza kutolewa kwa matibabu ya uvimbe au vipele vya namna hii na mtaalamu wa afya na baadhi ya nyakati mgonjwa hufanyiwa upasuaji kama tiba.
Kaswende
Vipele vya kaswende husababishwa na uambukizo wa bakteria Treponema pallidum anayeenezwa kwa kufanya ngono.
Sifa zake
Hutengeneza kidonda kigumu cha duara na kisicho na maumivu. Utahitaji matibabu mara moja kama utapatwa na dalili hii.
Tazama picha kwa maelezo zaidi
Sakabi
Hutokana na vimelea wadogo wanaochimba na kuingia chini ya ngozi hivyo kuonekana kama upele au uvimbe mdogo. Vimelea vya skabi huweza kutaga mayai chini ya ngozi na hivyo kupelekea muwasho mkali haswa wakati wa usiku.
Saratani
Ni kwa ndra sana upele kwenye ngozi ya uume unaweza kuashiria saratani.
Sifa zake
Upele wa saratani huweza kukua haraka, huwa na umbile lislilo na mipaka ya kueleweka na huweza kuwa na maumivu au la.
Wasiliana na daktari kwa uchunguzi kama unapata vipele vyenye sifa kama zilizotajwa hapo juu vilivyodumu kwa muda wa wiki nnje au zaidi kwa uchunguzi.
Chunusi
Ni vipele vidogo vinavyoweza kuwa na kichwa chenye mwonekao mweupe au mweusi vinavyosababishwa na kuziba kwa vitundu vya ngozi kutokana na mafuta, maambukizi ya bakteria, vinyweleo au uchafu kwenye ngozi.
Sifa zake
Huweza kuacha alama nyeusi au kovu kweney ngozi baada ya kupona na huchochewa sana na mabadiliko ya homoni au msongo wa mawazo.
CREDITS:ULY CLINIC