Muda sahihi kwa Mwanaume kufanya vipimo vya kuzuia saratani ya tezi dume
Kwa PSA, uchunguzi wa njia ya haja kubwa ni moja ya hatua zilizopendekezwa kwa uchunguzi wa saratani ya tezi dume
Linapokuja suala la kuzuia ugonjwa huu, kuna mikakati miwili kuu.
Mkakati wa unalenga kudhibiti sababu za hatari ambazo zinasababisha kuonekana kwa uvimbe, kama vile kutovuta sigara na kudumisha uzani wa mwili unaofaa katika maisha yote kupitia lishe ya kutosha na shughuli za kawaida za mwili.
Wa pili unahusu ugunduzi wa mapema wa saratani katika tezi hii ya mfumo wa uzazi, inayohusika na uzalishaji wa maji ambayo hutengeneza maji maji ya mbegu za uzazi na mbegu zenyewe.
Kwa miaka mingi, kampeni zinazohimiza uchunguzi wa uvimbe wa saratani za tezi dume ambazo zinaambatana na Mwezi wa Blue wa Novemba (Blue November)-kampeni inayowahamasisha wanaume wote wenye umri wa zaidi ya miaka 45 au 50 kumuona daktari wao na kuwa na vipimo vya digitali vya saratani ya korodani vya PSA.
PSA ambayo inamaanisha antijeni maalum ya saratani ya tezi dume, ni kimeng’enyo (enzyme) kinachopimwa katika. Ikiwa kimeng’enyo hicho kitazidi kikomo fulani kilichoanzishwa na wataalam, inaweza kuonyesha tatizo na tezi ya kiume.
Vipimo vya njia ya haja kubwa kidigital ni ni kipimo ambacho mtaalamu wa huduma ya afya huingiza kidole chake kwenye njia ya haja kubwa ya mgonjwa kugusa tezi dume (ni karibu na utumbo) na kuhisi iwapo kuna kitu chochote kisicho cha kawaida.
Majaribio haya , hata hivyo, yamehojiwa, kujadiliwa na kuwekwa katika mtazamo katika miaka ya hivi karibuni nchini Brazil na duniani kote.
Kwa upande mmoja, taasisi – kama vile Wizara ya Afya na Taasisi ya Saratani ya Taifa (Inca) – zinazuia uchunguzi wa mara kwa mara wa saratani ya tez idume.
Kwa upande mwingine, vyombo kama Jumuiya ya Urolojia ya Brazil (SBU) hutetea umuhimu wa kipimo hiki cha mara kwa mara kwa watu fulani.
Je, ni hoja gani zilizowasilishwa na pande zote mbili? Na, muhimu zaidi, wanaume wanapaswa kufanya nini kwa afya zao wenyewe ili kugundua uvimbe wa saratani ya tezi dume katika hatua ya mapema, wakati nafasi za kupona ni kubwa zaidi.
Taasisi ya Saratani ya Taifa ya Brazil inasema nini
Mwishoni mwa Oktoba, Inca na Wizara ya Afya walichapisha barua ya kiufundi inayohalalisha athari za uchunguzi wa wingi kwa saratani ya tezi dume.
Hoja kuu iliyowasilishwa katika maandishi ni hatari ya kutendewa vibaya – au kutumia rasilimali za matibabu bila ulazima na zaidi ya kile kinachohitajika, na hivyo kusababisha madhara kuliko faida za kipimo chenyewe.
Na hapa kuna maelezo: kati ya 30 na 40% ya tuvimbe ambao huonekana kwenye tezi dume huwa ya haukui kwa kasi bali huongezeka taratibu , tofauti na uvimbe wa saratani nyingine.
Katika hali ambapo ugonjwa hauna madhara, madaktari kwa ujumla wanapendekeza kufanya ufuatiliaji wa mgonjwa kwa kufanyiwa vipimo rahisi bila hitaji la kumuweka mgonjwa kwenye mpango wa matibabu au upasuaji.
Hatua hizi zinapitishwa tu ikiwa vipimo vinaonyesha mabadiliko katika hali hiyo, kama vile kukua haraka kwa uvimbe unaoweza kutishia maisha yake.
Hatari nyingine iliyoonyeshwa na wawakilishi wa mashirika yanayohusishwa na serikali ya shirikisho inahusishwa na biopsy. Kwa muhtasari, wagonjwa ambao wana mabadiliko makubwa katika uchunguzi wa PSA na / au digital rectal wanapaswa kupitia utaratibu ambao huondoa kipande kidogo cha sehemu ya uvimbe na kuukifanyia uchunguzi kwenye maabara ili kubaini iwapo una seli za saratani.
Tezi dume (mfano wa saratani ya tezi dume katika rangi nyekundu) iko chini ya kibofu cha mkojo (penye rangi ya njano) na ina jukumu la kuzalisha maji ya mbegu za uzazi
Lakini, kufuatia hoja hii, tunaweza kufanya nini ili kujilinda au kugundua saratani ya tezi dume mapema?
“Wanaume wanahitaji kuzuia sababu za hatari na kupitisha tabia nzuri, kama vile kupunguza matumizi ya pombe, kutovuta sigara na kujihusisha na shughuli za kimwili,” Maciel anajibu.
“Pia ni muhimu kuzingatia ishara na dalili na kupata huduma ya afya haraka. Ikiwa kuna kitu tofauti, ni muhimu kwenda kwenye kitengo cha afya na kuzungumza na mtaalamu ili kuanzisha utambuzi wa mapema iwezekanavyo wa uvimbe huu, “Anaongeza.
Miongoni mwa dalili zinazotia wasiwasi zilizotajwa na mtaalamu ni mabadiliko ya tabia za mkojo, ugumu au maumivu wakati wa kukojoa, pamoja na kuonekana kwa damu au kimiminika cha rangi ya waridi kwenye mkojo.
“Tunafuatilia ushahidi, hasa kwa sababu sayansi ina nguvu. Ikiwa utafiti utathibitisha vinginevyo na kuonyesha thamani ya ufuatiliaji, tutatathmini upya msimamo wetu, “anasisitiza Maciel.
“Tunapofikiria kuhusu afya ya umma, hatuwezi kufanya makosa. Kwa sababu mapendekezo yetu yanaathiri maisha ya mamilioni ya watu na lazima tuwe waangalifu sana,” anahitimisha.