Vyakula vyenye Mafuta Kidogo kupunguza hatari ya Saratani.
Kulingana na Tafiti Mpya,vyakula vyenye kiwango kidogo cha mafuta husaidia kupunguza hatari ya kupata Saratani ya Mapafu
Watafiti kutoka China walichambua data kutoka kwa kundi la zaidi ya watu 98,000 walioshiriki katika utafiti wa saratani nchini Marekani,
na wakagundua hatari ya chini ya asilimia 24% ya saratani ya mapafu kwa watu ambao walikuwa na kiwango kidogo cha mafuta katika lishe yao.
Kupungua huku kulionekana zaidi kwa asilimi 29% Ya wavutaji sigara ambao walikuwa na lishe yenye kiwango cha chini cha mafuta.
Matokeo haya yaliripotiwa katika Jarida la Lishe, Afya na Uzee. Kwa ujumla, wanapendekeza kwamba vyakula vilivyojaa mafuta mengi vilihusishwa na ongezeko la asilimia 35% ya hatari ya Saratani ya mapafu, kwa ujumla, na hatari maradufu ya kansa ya mapafu ya seli ndogo.