DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO NA MAMA BAADA YA KUJIFUNGUA

  ZIPO DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO NA MAMA BAADA YA KUJIFUNGUA

➡️ Ombeni Mkumbwa


(1) DALILI ZA HATARI KWA MJAMZITO

-Mama mjamzito kuvimba miguu,uso na mikono

-Mama mjamzito kuona maruerue

-Kuvuja damu

-Mama mjamzito kuwa na presha kubwa na kuwepo kwa protein kwenye mkojo wake kwani hiki ndicho kiashiria kikubwa cha kwanza cha uwepo wa ugonjwa wa KIFAFA CHA MIMBA

-Mtoto kutokucheza tumboni kwa zaidi ya masaa 24 kwa mama ambaye mimba imefika umri wa mtoto kucheza tumboni

-Chupa ya Uzazi kupasuka kabla ya mda wa kujifungua kufika

-Mjamzito kutokwa na uchafu wenye harufu kali pamoja na miwasho ukeni,mkojo kuuma wakati wa kukojoa hizi ni dalili za magonjwa kama FANGASI,UTI, PID n.k.

(2)DALILI ZA HATARI KWA MAMA BAADA YA KUJIFUNGUA


-Kujuva damu nyingi baada ya kujifungua kuanzia masaa 24 mpaka wiki 6, Hivi ni dalili za ugonjwa unaitwa POSTPARTUM HEMMORGE (PPH)

-Kupatwa na kizungu zungu pamoja na kuona maruerue

-Kuvimba miguu,uso na mikono kupita kiasi.

KWA DALILI KAMA HIZI TAFTA MSAADA KWA WATAALM WA AFYA ILI UPATE MSAADA.

 ATHARI ZA GROUP LA DAMU NEGATIVE KWA MJAMZITO

➡️ Ombeni Mkumbwa


Soma hii ili kuelewa juu ya Group la damu NEGATIVE...

Mama mjamzito ambaye ana Group la Damu Negative yaani Mfano; Group A rhesus factor NEGATIVE (A-), ikiwa Mwanaume aliyepata naye Ujauzito ni Group la Damu Positive Mfano; Group A rhesus factor POSITIVE (B+).

 Yupo kwenye hatari ya kumpoteza mtoto aliyemzaa hasa Ujauzito wa Pili, au yupo kwenye hatari ya kupata mimba na kutoka zenyewe.

ANGALIZO

Kwahyo basi kama Mjamzito imegundulika ana tatizo hili la Kuwa na Kundi la Damu Negative(Blood group Negative) ni vizuri ihakikishwe amechomwa sindano ijulikanayo kama ANT-D injection ili kumsaidia mama huyu asipate madhara niliyoyataja Hapo juu.


JUKUMU LANGU KWAKO NI KUKUPA USHAURI,ELIMU AU MSAADA WA KIAFYA PALE INAPOHITAJIKA.
   

  Tuma ujumbe kwa namba +255758286584 kama unahitaji Ushauri,elimu au msaada juu ya afya yako.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!