Ticker

6/recent/ticker-posts

FAIDA YA USINGIZI PAMOJA NA NJIA 13 ZA KUPATA USINGIZI MZURI



  FAIDA YA USINGIZI PAMOJA NA NJIA 13 ZA KUPATA USINGIZI MZURI

➡️ Ombeni Mkumbwa

Japokuwa kadri umri unavyokuwa Mkubwa ndivo masaa ya kulala hupungua,ila bado umuhimu wa kulala vizuri ni Mkubwa sana, Tafiti Zinaonyesha Mtu anayepata usingizi au anayelala vizuri,Mfano kwa Mtu Mzima wastani wa masaa 8 yanatosha kabsa,Humsaidia sana katika vitu vitu mbali mbali.

SUMMARY

Katika Makala hii tunajadili Faida za kupata Usingizi Mzuri na Njia 13 za kukusaidia wewe mwenye matatizo ya kukosa usingizi kila siku,kutatua tatizo hili kwa haraka sana.Na kuendelea kufurahia Maisha.

 

Baadhi ya Faida za kupata Usingizi Mzuri ni pamoja na hizi hapa;

  • Kuimarisha Kinga yake ya Mwili
  • Kuongeza Uwezo wake wa akili pamoja na uwezo wake wa Kufikiri Vizuri
  • Huondoa uchovu wa Mwili pamoja na kuupa mwili Nguvu ya Kutosha
  • Huleta Ngozi ya mwili kunawiri pamoja na afya ya seli Hali za mwili

NJIA 13 ZA KUKUSAIDIA KUPATA USINGIZI MZURI

Zifuatazo ni Njia ambazo zitakusaidia wewe kwa kiasi kikubwa kupata Usingizi mzuri na kuleta Nguvu na si uchovu katika Mwili wako;
  1. Punguza Matumizi ya mwanga wa Blue au vitu venywe mwanga wa blue wakati wa siku,kama vile kwenye Taa au simu. Tafiti zinaonyesha kwamba mwanga wa Blue hupunguza uzalishaji wa Homoni au kichocheo aina Ya Melatonin ambacho ndyo huhusika na kuleta Usingizi.
  2. Kaa kwenye Mwanga wa Kutosha wakati wa Mchana, Hii husaidia mwili wako kuweza kutofautisha wakati wa usiku ni upi na wakati wa Mchana ni upi,hivo kukusaidia wewe kupata usingizi mzuri wakati wa usku.
  3. Matumizi ya Vinywaji vyenye Caffeine hasa wakati wa Usiku huuchangamsha mwili wako na kukusababishia kukosa Usingizi kabsa wakati wa Usku. Hivo epuka matumizi haya ya Vinywaji vyenye Caffeine wakati wa Usku.
  4. Punguza tabia ya kulala wakati wa mchana,hii itakusaidia wewe kulala vizuri wakati wa Usku.
  5. Inashauria kwa asilimia kubwa muda wa kulala na kumka kila siku uzingatiwe sana,hali hii huuzoesha mwili kwamba sasa ni wakati wa usku na ni wakati wangu wa kulala.
  6. Epuka matumizi ya pombe au kilevi chochote,kwani hivi huathiri uzalishaji wa kichocheo au homoni hii ya Melatonin ambayo inahusika na Usingizi moja kwa moja.
  7. Boresha Mazingira yako ya kulala,Tafiti zinaonyesha watu wengi wanaosumbuliwa na matatizo ya kukosa Usingizi, hulala kwenye vyumba ambao si rafiki mfano,Chumba ambacho kina mwanga sana,chumba chenye Joto sana,Chumba chenye baridi sana,Chumba ambacho kina makelele ya aina yoyote,mfano Redio au watu.
  8. Epuka matumizi au ulaji mwingi wa chakula wakati wa usiku,pia Epuka kula vyakula vizito sana wakati wa Usku.
  9. Pumzisha akili yako na iburudishe na vitu  kama Mziki laini n.k kabla Ya kulala na epuka kutazama vitu kama Movies ndefu za kutisha wakati wa usku
  10. Hakikisha umeoga kabla ya kwenda kulala Au kuupumzisha mwili wako kitandani.
  11. Tumia godoro zuri na mto safi kama wewe ni mpenzi wa mto wakati wa kulala, Kulala chini au kwenye kamba n.k,ni ngumu sana kupata usingizi mzuri
  12. Fanya mazoezi kila siku wakati wa mchana kabla siku yako haijaisha au kabla hujaenda kulala kitandani
  13. Epuka kunywa kwa wingi vimiminika,kwani vitakufanya uanze kuamka amka mara kwa mara wakati wa usku,hivo kupelekea kukosa usingizi mzuri.
@KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584 TUMA UJUMBE AU PIGA SIMU UTASIKILIZWA NA KUHUDUMIWA KWA HARAKA POPOTE ULIPO.





Post a Comment

0 Comments