FAIDA ZA KUTUMIA MICHAICHAI MWILINI
FAIDA ZA MICHAICHAI MWILINI
Ukitaka kuwafukuza Mbu wanaoleta ugonjwa wa Malaria nyumbani kwako panda Mmea wa Mchaichai au weka huo Mmea ndani ya nyumba yako kama pambo basi Mbu hawata sogea nyumbani kwako utakuwa umewaweza Mbu wana uchukia huo Mmea wa Mchaichai. Haya nimewapeni Dawa ya bure hiyo kazi kwenu.
FAIDA YA KUTUMIA MCHAICHAI KAMA TIBA NA CHAKULA
Faida za mchachai zipo nyingi sana wengi wetu hudhani mchaichai ni kiungo cha kuweka kwenye chai pekee, au ni dawa kwa ajili ya kuua mbu pekee, ila mchaichai huwa na faida lukuki zaidi ya hizo tu. Naomba uweze kusoma makala haya ili uone faida nyinginezo za mchaichai.
Zifuatazo ni faida za kutumia mchaichai kiafya.
1. Mchaichai ni kinga dhidi ya saratani.
Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa kwenye kila gram 100 ya mchaichai, kuna viondosha
sumu ambavyo vina uwezo wa kuukinda mwili dhidi ya ugonjwa wa saratani. Mwaka 2006, timu ya watafiti kutoka Chuo kikuu cha Gurion, Israel waligundua mchaichai una uwezo wa kuua seli zinaweza kusababisha saratani.
2. Hutibu magonjwa ya kuhara.
Husaidia umeng’enyaji wa chakula Chai ya mchaichai hurahisisha utaratibu wa mmeng’enyo wa chakula na pia hutibu magonjwa ya kuhara na maumivu ya tumbo ikiwamo kujaa gesi.
Hurahisisha utaratibu wa kuondoa uchafu mwilini Katika matibabu, unatibu magonjwa mengi ikiwemo kushusha joto, hasa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na malaria kali.
3. Husaidia kusafisha figo na mkojo.
Mchaichai pia una kazi ya kusafisha figo ambayo kazi yake kubwa ni kusafisha damu mwilini, kuondoa mafuta mabaya mwilini ambayo mengi yanatengenezwa na kemikali kiwandani na hivyo mwili kushindwa kuziondoa na baadaye kusasababisha magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani.
Figo inapokuwa safi na imara, hata kazi nyingine kama kusafisha mkojo zinafanyika kirahisi kwani mkojo unapozidi kuwa mchafu mtu hujikuta akivimba mwili na wakati mwingine kufikia hata hatua ya kupoteza maisha.
4. Hupunguza maumivu wakati wa hedhi.
Mchaichai pia huwasaidia kina mama ambao wanaumwa na tumbo kipindi cha hedhi, ambao wengi wao huchukulia kama chango.
“Unapokunywa mchaichai, unawezesha kusafisha mirija ya uzazi na hivyo kuwezesha damu kupita kwa urahisi,”
Cc:afyasolution #afyaclass
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!