FAIDA ZA MATUMIZI YA ASALI KWA WANAUME

ASALI KWA MWANAUME

Mwanamme anayetumia asali mara kwa mara anakuwa na faida tatu katika afya yake ya uzazi

.

.

1;MBEGU ZA KIUME

Mbegu za kiume huhitaji nguvu zinazozalishwa na sukari za frucose ili ziweze kuogelea vizuri na kupambana na hali ngumu iliyopo kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke.Asali ni miongoni mwa vyakula bora kabisa vyenye wingi wa sukari hii.Kumbuka kuwa tofauti na viungo au sehemu zingine za mwili ambazo hutumia glucose kama chanzo cha nguvu zake,mbegu za kiume hutumia fructose tu ambayo unaweza kuipata pia kwenye matunda

.

.

2;NGUVU ZA TENDO LA NDOA

Tendo la ndoa huhitaji nguvu za kutosha kulitimiza kikamilifu.Asali huwa ni chanzo bora kabisa cha nguvu.Kijiko kimoja cha asali kinatosha kukupa idadi ya calories 64 za nguvu,huku gramu 100 za asali (vijiko vitano) vikikupa zaidi ya calories 304 za nguvu ambazo zinaweza kukufanya uwe mwanamme usiye na mashaka katika ufanisi wa kazi zako (tendo la ndoa)

.

.

3;UTENGENEZWAJI WA MBEGU BORA ZA KIUME

Ili uwe na uwezo wa kurutubisha yai (kutungisha mwanamke ujauzito) unahitaji mbegu zenye maumbo mazuri,zilizo na kasi kubwa ya kuogelea pamoja na afya bora.Ulaji wa asali utakupa faida hizi tatu zote kwa pamoja

#afyadarasa

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!