FAIDA ZA TUNDA LA TIKITIKI MAJI
Tikitimaji linapokuwa limeiva huwa na utajiri wa kemikali inayoitwa glutathione.Kemikali hii huongeza mara dufu kinga ya mwili hivyo kuongeza uimara wa mfumo wa mwili katika kupambana na magonjwa.Ili upate glutathione kwa wingi,inatakiwa utumie sehemu nyekundu ya tunda hili inayokaribiana na gamba lake la nje.Hapo ndipo hupatikana kwa wingi.
-
Pia huwa na Amino acid zinazojulikana kama citrulline ambazo hupanua mishipa ya damu hasa ile inayopatikana kwenye viungo vya uzazi (kwa wanaume).Hufanya kazi kama zilivyo viagra hivyo huitwa viagra asili.Tunda hili linaweza kusaidia kuboresha afya ya uzazi kwa wanaume walio na matatizo katika kushiriki tendo la ndoa (upungufu wa nguvu za kiume)
-
KAZI ZINGINE
Huwa na beta cryptoxanthin ambayo hupambana na uvimbe mwilini,huongeza uwepo wa maji mwilini,huboresha afya ya moyo,hupambana na kutoa kinga dhidi ya aina mbalimbali za saratani mwilini,hupunguza uchovu na kukaza kwa misuli pamoja na kuboresha afya ya macho
Cc:afyainfo
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!