HARUFU MBAYA MDOMONI

JE UNASUMBULIWA NA TATIZO LA HARUFU MBAYA MDOMONI?

➡️ Ombeni Mkumbwa

Watu wengi Hawajui kwamba kunuka Mdomo ni tatizo japo pia kutokusafisha vizuri Mdomo hasa kupiga Mswaki huweza kusababisha Mdomo wako kunuka.

SABABU ZA MDOMO KUTOA HARUFU MBAYA

Zipo Sababu mbalimbali ambazo huweza Kusababisha Mdomo wako Kunuka na kuwa kero kwa Watu hasa wakati wa kuongea.

1. Maambukizi ya Magonjwa kama Fangasi wa Mdomoni na kwenye Ulimi, ni miongoni mwa sababu kubwa za Mdomo kutoa Harufu mbaya.

2. Kutokusafisha kinywa Vizuri,hasa hasa kuacha kupiga Mswaki asubuhi ukiamka, na baada ya Mlo au Chakula.

3. Arufu ya Vitu kama vitunguu kutoka Mdomoni hasa hasa kwa wale wanaopenda kutafuna Vitunguu ambavyo ni vibichi.

4. Pia mtu huweza kutoa harufu mbaya mdomoni kama yupo kwenye Matumizi ya dawa zinazohusu mdomo,mfano dawa mbali mbali za Kutibu meno n.k

MATOKEO;

➖ Kwa mtu ambaye hasafishi meno vizuri yupo kwenye hatari kubwa ya kupatwa na Tatizo la Meno kuuma,hivo ni baada ya jino pamoja na Fizi kushambuliwa na wadudu mbali mbali ikiwemo bacteria wanaongia na kutoboa meno au fizi za Mhusika.

➖ Tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni huweza kuwa kero kubwa kwa watu wengine,hivo kupelekea jamii kukutenga na kukusema vibaya hata kama tatizo lako halitokani na uchafu wa kinywa bali ni Ugonjwa kama maambukizi ya Fangasi Mdomoni.

MATIBABU YA TATIZO

Ni vizuri sana kwa Mtu mwenye tatizo hili kwenda hospital kwa ajili ya Uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha tatizo lake,Kwani matibabu ya tatizo hili huanza pale tu chanzo chake kinapojulikana kwanza.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!