JE KUVUJA DAMU MAPEMA KATIKA UJAUZITO NI NINI?

 Je, kuvuja damu mapema katika ujauzito ni nini?


Kuvuja damu kabla ya wiki 28 za ujauzito hudhaniwa kuwa ni kuvuja damu mapema katika ujauzito. Ikitokea baada ya wiki 28, huitwa utokaji wa damu wa baadaye katika ujauzito. 

.

Mgawanyo huu wa wiki 28 umezingatia uwezekano wa kuishi ikiwa mtoto atazaliwa kabla ya tarehe iliyotarajiwa katika wiki 28. Matumaini ya kuishi kabla ya wiki 28 ni madogo sana katika nchi nyingi zinazoendelea maana kuna upungufu wa vifaa vya afya vya utunzaji maalum kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.

.

 Siku hizi nchi zingine zimepunguza mgawanyo huu hadi wiki 20 kwa sababu ya utunzaji ulioimarishwa na teknolojia inayotolewa na mfumo wao wa afya.


Visababishi vikuu vya kuvuja damu mapema katika ujauzito ni 

-utokaji wa mimba au mimba kutishia kutoka.

 -mimba iliyotungwa nje ya kizazi au uterasi (hapa mtoto hujishikiza na kukua nje ya kizazi au uterasi),

-Uvimbe kwenye kizazi

-Kondo la nyuma au placenta kuachia ambapo kitaalamu huitwa (placenta abruption)

-Kondo la nyuma kushuka chini hali inayojulikana kama Placenta previa

-Mama mjamzito kupigwa au kuanguka na kupelekea mshtuko kwny tumbo la uzazi n.k

#kuvujadamu

#Mjamzito 

#ombenimkumbwa

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!