JINSI YA KUPATA WATOTO MAPACHA (TWINS)
➡️ Ombeni Mkumbwa
☑️SUMMARY
📶 SOMO KAMILI
Watoto mapacha ni nini?
•Watoto mapacha (TWINS)- ni watoto wawili ambao wanazaliwa wakati mama anajifungua, ambapo wanaweza kuwa watoto wa jinsia moja yaani wanawake Wote au wanaume wote,au wakawa wa jinsia tofauti yaani mwanamke na mwanaume.
AINA ZA MAPACHA
Kuna aina mbili za mapacha,nazo ni kama ifautavyo;
(1) Mapacha wanaofanana au kitaalam huitwa Identical Twins- mapacha hawa kama lilivyo jina lao kwa asilimia kubwa hufanana vitu vingi mfano Group lao la Damu, Jinsia- kama ni wakike wote wanakuwa wakike na kama ni wakiume wote basi wanakuwa wakiume
(2) Mapacha wasiofanana au kitaalam huitwa Fraternal Twins- na hawa kama lilivyo jina lao kwa asilimia kubwa wanakuwa na vitu vinatofautiana Mfano Jinsia kama mmoja ni wakike mwingine ni wakiume,group lao la damu n.k
JINSI MAPACHA HAWA WANAVYOTOKEA
kwanza tuwekane sawa hapa; Ili Ujauzito utokee lazima mbegu ya mwanaume iweze kulikuta Yai linalotoka katika vifuko vya Mayai vya mwanamke yaani OVARIES,ifanikiwe kuingia ndani na kulirutubisha Yai hilo,ambapo kwa asilimia kubwa urutubishaji huo hutokea katika mirija ya uzazi yaani Fallopian Tubes, Hapo ndipo ujauzito hutokea na safari ya mtoto kuzaliwa huanzia hapo.
(A) Mapacha wanaofanana au Identical Twins jinsi wanavyotokea- Mbegu moja ya mwanaume kufanikiwa kulikuta yai moja la mwanamke,kuingia ndani na kulirutubisha,ambapo baada ya urutubishaji lile yai hugawanyika mara mbili,hapo ndipo mapacha wanaofanana hutokea.
(B) Mapacha wasiofanana au Fraternal Twins- Aina hii ya mapacha(Twins) hutokea pale ambapo mbegu mbili za mwanaume zimefanikiwa kuyakuta mayai mawili kutoka katika vifuko vya mayai ya mwanamke yaani OVARIES,kuingia ndani, na kuyarutubisha hayo mayai mawili,Hapa ndipo watoto mapacha wasio fanana hutokea au Kitaalam tunasema Fraternal Twins.
JINSI YA KUGUNDUA KAMA UNA MAPACHA
✓Kipimo cha Ultrasound, kipimo hiki husaidia kujua kama mjamzito ana watoto mapacha au mtoto mmoja tumboni
✓Kupimwa na wataalam wa afya kwa kusikiliza mapigo ya moyo ya mtoto tumboni kwa kutumia kifaa maalum kijulikanacho kama FETOLSCOPE
✓Mjamzito kuwa na tumbo kubwa kupita kiasi,Japo sio kila tumbo kubwa basi ni watoto mapacha,wengine ni matatizo kama,Tatizo la Big baby(Mtoto mkubwa sana tumboni), Tatizo la kujaa maji ya uzazi na matatizo mengine kama hayo
✓Mama anapojifungua,hapo ndyo ukwel wa mambo yote utajulikana, kwamba je mtoto ni mmoja au ni mapacha
Kumbuka; Watoto wakiwa watatu sio TWINS tena bali huitwa TRIPLETS, na uwezekano wa kuzaa watoto mapacha ni mkubwa kuliko uwezekano wa kuzaa watoto watatu kwa wakati mmoja
VITU VYA KUZINGATIA ILI MTOTO AWE NA AFYA BORA
➡️ Ombeni Mkumbwa
KWA USHAURI ZAIDI/ ELIMU/ TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584 UPATE MSAADA,UKITUMA UJUMBE UTAHUDUMIWA KWA HARAKA ZAIDI
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!