JINSI YA KUPUNGUZA UZITO

  JINSI YA KUPUNGUZA UZITO NA MADHARA YA KUWA NA UZITO MKUBWA AU UZITO ULIOPITILIZA

➡️ Ombeni Mkumbwa

🔻SUMMARY

Mada ambazo tumejadili katika makala hii zinagusa maeno haya yafuatayo;

(1) Utangulizi na tafiti mbali mbali ikiwemo kutoka WHO-shirika la afya Duniani

(2) Jinsi ya kutambua kama Una uzito mkubwa au uzito uliopitiliza

(3) Range za kila uzito pamoja na Tafsiri zake

(4) Madhara ya Kuwa na Uzito mkubwa

(5) Jinsi ya kupunguza Uzito uliopitiliza au uzito mkubwa

📶 SOMO KAMILI

Utangulizi;

Kutokana na Shirika la Afya Duniani yaani "World health Organization(WHO), limetaja kuwa na Ongezeko kubwa la Watu wenye uzito uliopitiliza siku hizi na kuhusisha moja kwa moja na Ongezeko la watu wenye  Magonjwa ya Moyo,kisukari,Ini na Presha Duniani.

Huku WANAWAKE wakiwa ni Miongoni mwa Kundi kubwa lililokumbwa na Tatizo hili la Kuwa na Uzito mkubwa au Uzito uliopitilisha.
Vitu ambavyo Vimeshauriwa na wataalam wa afya juu ya tatizo Hili ni pamoja na; 
(1)Kufanya Mazoezi ili kupunguza Uzito wa mwili
(2)Lishe au kula vyakula ambavyo havisababishi uzito wako kuongezeka zaidi

JE UTAJUAJE KAMA UNA UZITO MKUBWA AU UZITO ULIOPITILIZA?

Jifunze hapa Jinsi ya kupima Uzito wako;

Kupima uzito wako,Tunatumia kitu kinaitwa (BMI) yaani Body Mass Index

Hiki ni kipimo kinachotumia urefu na uzito wako kujua Kama una uzito sahihi unaotakiwa kiafya. Au Tumia BMI calculator ili kupata majibu sahihi na kwa haraka zaidi

  BAADA YA KUPATA MAJIBU YAKO ANGALIA KAMA YAPO KWENYE KUNDI LIPI KATI YA HAYA.

Ikiwa BMI yako ni:
* Chini ya 18.5- una Uzito mdogo au underweight.
* Kati ya 18.5 na 24.9 - una uzito sahihi kwa afya .✔️
* Kati ya 25 na 29.9 - una uzito mkubwa yaani overweight.
* Kutoka 30 Na zaidi -una uzito uliopitiliza.

Adult Body Mass Index (BMI)

If your BMI is less than 18.5, it falls within the underweight range. If your BMI is 18.5 to <25, it falls within the normal. If your BMI is 25.0 to <30, it falls within the overweight range. If your BMI is 30.0 or higher, it falls within the obese range. Source Ya Taarifa Hii Soma Hapa...!!!

MADHARA YA KUWA UZITO MKUBWA AU ULIOPITILIZA

Haya ni baadhi ya madhara kwa watu wenye uzito mkubwa au uliopitiliza;
1.Kupata Matitizo kwenye figo
2.Uwepo wa michirizi kwenye Ngozi
3.Hamu ya tendo la ndoa kupungua
4.Mfumo mzima wa upumuaji kuharibika
5.Kuharibu kiungo Muhimu "INI"
6.Hupelekea uwezekano wa kupata kisukari,tatizo la presha na Gauti
7.Magonjwa kwenye mfumo wa moyo
8.Kuleta shida kwenye mfumo wa ubongo
9.Kasi ya kuishi hupungua
10.Kupata shida kwenye mmeng'enyo wa chakula
11.Maumivu kutokea kwenye viungo kama vile kiuno na Magoti.
12.Kiwango cha mafuta mwilini kuongezeka kwa kasi

🔷 JINSI YA KUPUNGUZA UZITO MKUBWA

Zipo njia nyingi sana za kupunguza uzito siku hizi,na hii ni kutokana na tatizo hili limekuwa likiwasumbua watu wengi sana katika maeneo tofauti tofauti. Mimi nataka kukupa Tips ambazo zinaweza kukusaidia katika tatizo hili na uzito wako ukawa wa kawaida na ukaweza kuepuka kupata magonjwa yanayohusishwa moja kwa moja na uzito kuzidi.

➖ Jijengee tabia ya kufanya mazoezi kila siku, na ukiweza waone kabsa wataalam wa mazoezi ya kupunguza Uzito,hii itakusaidia sana kwa asilimia kubwa kutatua tatizo hili la uzito kuwa mkubwa au kupitiliza.

➖ Hakikisha unazingatia kanuni na taratibu za Ulaji, hasa hasa kuepuka sana vyakula vya mafuta sana,na vyakula vyenye protein sana kwani hii huongeza uzito kwa kasi sana

➖ Epuka matumizi ya dawa kiholela bila kufata wataalam husika wa afya,kwani hii inaweza kuongeza ukubwa wa tatizo na sio kupunguza Tatizo lako.

➖ Tafiti zinaonyesha kwamba mchezo kama Mpira wa miguu hupunguza tatizo hili kwa asilimia kubwa sana.

Kumbuka

Kwa hivi sasa wanawake wamekuwa wahanga wa kubwa sana wa tatizo hili la kuwa na uzito mkubwa au uzito kupitiliza ikilinganishwa na wanaume.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU MSAADA WA KIAFYA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584 PIGA AU TUMA UJUMBE UTAHUDUMIWA.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!