KITOVU CHA MTOTO BAADA YA MAMA KUJIFUNGUA.

 🔻MAMBO YA KUZINGATIA KWENYE KITOVU CHA MTOTO BAADA YA KUZALIWA

➡️ Ombeni Mkumbwa

Baada ya mama kujifungua kitovu cha mtoto hukatwa na kutenganisha mawasiliano kati yake na mtoto,hivo mtoto kujitegemea mwenyewe.

YAPO BAADHI YA MAMBO MUHIMU SANA YA KUZINGATIA KUHUSU KITOVU CHA MTOTO

1-Mama hakikisha kitovu cha mtoto hakivuji damu baada ya kukatwa na kufungwa na mtaalam wa afya.

2-Kitovu hudondoka chenyewe,ambapo kwa asilimia kubwa kwa watoto wengi ndani ya wiki moja,kitovu huwa tayari kimeshadondoka.

3-Hakikisha kitovu cha mtoto hakitoi usaha,au kubalika rangi hasa ya manjano na kutoa harufu mbaya,hii sio dalili nzuri.

4-Usiweke kitu chochote kwenye kitovu cha mtoto mpka kidondoke chenyewe.

5-Epuka imani potofu kama zile za kuweka mavi ya Ng'ombe n.k,kwenye kitovu cha mtoto.

KWA USHAURI,ELIMU AU MSAADA WA KIAFYA MAWASILIANO NI +255758286584.


KUMBUKA; JUKUMU LANGU KWAKO NI KUKUSHAURI,KUKUELMISHA NA KUKUPA MSAADA WA KIAFYA PALE INAPOHITAJIKA.

Karibu Sana..!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!