MAKOSA YANAYOFANYWA KATIKA KUCHAGUA AINA ZA PEDI PAMOJA NA MATUMIZI YAKE

➖ MAKOSA YANAYOFANYWA KATIKA KUCHAGUA AINA ZA PEDI PAMOJA NA MATUMIZI YAKE

1. Kutonawa mikono kabla na baada ya kutumia pedi. Mikono hushika sehemu mbalimbali  hivyo kuna uwezekano ikawa na vimelea vinavyosababisha magonjwa kwa hiyo kushika pedi bila kunawa mikono kwa sabuni kunaweza kuhamisha vimelea hivyo kutoka mikononi na kwenda kwenye pedi inayotegemewa kuvaliwa.


2. Kutunza pedi bafuni au chooni. Wadada wengi hupendelea kutunza pedi zao chooni/bafuni.


3. Kutoangalia muda wa matumizi wa pedi kabla ya kutumia au baada ya kuzihifadhi kwa muda mrefu hali inayopunguza kiwango cha ufanisi.


4. Kununua pedi zinazouzwa kiholela kwa njia ya utangazaji na za bei rahisi (promotion) ambazo baadhi zimeonekana kutengenezwa kwa malighafi zilizo chini ya kiwango au kukaa kwa muda mrefu hivyo kuuzwa kwa bei rahisi ili zitoke na kutumika haraka kabla ya kuisha muda wake.


5. Kutumia pedi moja kwa muda mrefu


6. Kupendelea pedi zenye uwezo mkubwa wa kufyonza unyevunyevu ili ivaliwe muda mrefu pia ni tatizo sababu kwa kadri muda wa kuvaa pedi moja unapozidi kuongezeka na hatari za maambukizi ya magonjwa pia inazidi kuongozeka.


#afyabongo #drtareeq


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!