MAMBO MUHIMU KWA MTOTO BAADA YA KUZALIWA MPAKA ATAKAPOFIKISHA UMRI WA MIAKA MITANO
MAMBO MUHIMU KWA MTOTO BAADA YA KUZALIWA MPAKA ATAKAPOFIKISHA UMRI WA MIAKA MITANO.
Katika hali ya kuhakikisha afya ya mtoto inaimarika kuna vitu vya muhim vya kuzingatia sana,Leo nitagusia baadhi ya vitu hivo;
(1)KUPATA CHANJO ZOTE MUHIMU mfano; kuna chanjo ya kuzuia kifua kikuu BCG,chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kupooza POLIO, chanjo za kuzuia mtoto kuharisha ROTAX, vitamin A, DAWA za MINYOO n.k.
(2)LISHE KWA MTOTO,hapa nazungumzia swala nzima la unyonyeshaji kwa MIEZ 6,ambao unahusisha maziwa ya mama peke yake ili kuzidi kuimarisha kinga ya mwili kwa mtoto, KWANI Kinga ya mwili kwa mtoto dhidi ya magonjwa hutokana zaidi na maziwa ya mama katika kipindi hiki.
(3)BAADA YA MTOTO KUZALIWA,USIWEKE KITU CHOCHOTE KWENYE KITOVU CHA MTOTO,kuna baadhi ya watu wenye iman potofu,hadi wengine hufikia hatua ya kupaka MAVI ya Ng'ombe kwenye kitovu cha mtoto.Hii ni hatari sana kwa afya ya Mtoto,Usiweke ktu chochote mpka kitovu kidondoke chenyewe.
(4)USAFI WA MWILI,Hakikisha mtoto unamsafisha vizuri
(5)NGUO ZA KUZUIA BARIDI,mvalishe mtoto au mfunike ili kuepuka hali ya baridi kwa mtoto;Kwani baridi kwa mtoto huweza kumsababishia kuumwa.
KUMBUKA;JUKUMU LANGU NI KUKUSHAURI,KUKUELIMISHA NA KUKUPA MSAADA WA KIAFYA PALE INAPOHITAJIKA. MAWASILIANO +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!