Tatizo ambalo linatokana na Maji kujaa kwenye mapafu, linahitaji matibabu ya haraka na wakati mwingine lisipozibitiwa vizuri huweza kusababisha kifo.
🔻DALILI ZA TATIZO HILI LA MAPAFU KUJAA MAJI
Ishara na dalili za kujaa Maji kwenye mapafu zinaweza kuonekana ghafla au kutokea baada ya muda. Ishara na dalili hizo ni pamoja na;
(1) Dalili za Awali
- Kupata Shida wakati wa kupumua (dyspnea) au kupumua kwa pumzi kali
- Hisia ya kukosa hewa au kuzama ambayo hutokea wakati wa kulala
- Kikohozi ambacho ni kikali na kinachoweza kuambatana na kutokwa na damu
- Kuhisi baridi kwenye Ngozi ya mwili
- Mapigo ya moyo kwenda mbio
(2) Dalili za Mda Mrefu
Ishara na dalili za mapafu ya muda mrefu (sugu) ni pamoja na;
- Ugumu wa kupumua wakati umelala
- Kupata kikohozi hasa wakati wa Usku ukiwa umekaaa
- Kupumua kwa pumzi kuliko kawaida wakati unafanya kazi
- Kuongezeka uzito kwa haraka
- Kuvimba Miguu pamoja na Uchovu wa mwili
VIPIMO;
- Ni pamoja na Picha Kifua (X-ray)
- Ultrasound ya Kifua
- Vipimo vya Damu
- Thoracentesis
- CT-Scan
MATIBABU
Kama Una dalili hizi au Una tatizo hilo ni vizuri kufika Hospital haraka kwa Ajili ya Uchunguzi na Kupata Matibabu sahihi kulingana na tatizo lako au chanzo cha tatizo lako.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!