MATATIZO YA HEDHI KWA MWANAMKE PAMOJA NA TIBA YAKE

MATATIZO YA HEDHI KWA MWANAMKE PAMOJA NA TIBA YAKE

➡️ Ombeni Mkumbwa

Wanawake wengi wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo mbali mbali yanayohusu hedhi, na wengi wao hawapati tiba sahihi kutokana na Matatizo yao.Leo nmejaribu kutaja matatizo baadhi ya Hedhi,na kila tatizo lina matibabu yake.Hivo pia nimetoa maelekezo jinsi ya kupata msaada mwisho wa Orodha ya matatizo hayo.

KUMBUKA: Afya yako ndyo Mtaji wako

MATATIZO YA HEDHI NI KAMA IFUATAVYO


1.kuumwa na Tumbo sana wakati wa Hedhi

2.Kuvuja Damu nyingi na kwa mda mrefu mfano wiki moja,mbili n.k

3.Kublid mara mbili au zaidi kwa Mwezi

4.Kukaa zaidi ya mwezi mmoja bila kupata Hedhi

5.Kupata hedhi ya mabonge mabonge,nyeusi na wengine kunatoka vipande kama vya maini.




CR: @Dr. Norman Jonas 🔻:

Kupata hedhi kupita kiasi ni moja ya matatizo ya uzazi yanayosumbua wanawake wengi. Tafiti zimeonyesha kwa kila wanawake 1000; wanawake 53 kati ya huwa na tatizo la kupata hedhi kupita kiasi. Ni theruthi tu ya wanawake wenye shida ya hedhi hutafuta tiba stahiki kwa daktari wengi hukaa nayo kwa aibu au hofu.

Makala hii nimegusia katika lugha rahisi visababishi vya hedhi kutoka nyingi ili itoe mwanga kwa wanawake kutafuta tiba pale wanapokabiriwa na changamoto hii

Je ni wakati gani mwanamke anatakiwa kuhisi kuwa anapata hedhi kupita kiasi?

  • Unapata hedhi inayozidi siku 7
  • Unapata hedhi nzito inayofanya ubadiri pedi moja ndani ya masaa mawili
  • Unapata hedhi nzito inayokulazimu kuvaa pedi zaidi ya moja
  • Unapata hedhi nzito inayolowesha hadi nguo za nje
  • Unapata hedhi nzito inayokulazimu kuamka usiku kubadiri pedi
  • Hedhi inayotoka na mabonge

Sababu gani huweza kuchangia mwanamke kupata hedhi nzito kupita kiasi?

Vivimbe kwenye kuta za mji wa kizazi; vivimbe hivi sio saratani huitwa fibYai kupevuka bila mpangilio (Irregular ovulation) ; hali hii husababisha kuta za mji wa mimba zivimbe na kuwa nene hivyo kutoa damu nyingi. Hutokea zaidi kipindi cha kuvunja ungo na kipindi cha kukaribia ukomo wa hedhi
  • Matatizo ya kugandisha damu
  • Matumizi ya dawa za kuzuia damu kuganda
  • Baadhi ya wanawake waliotumia vitanzi (IUD) hasa ndani ya mwaka wa kwanza
  • Maambukizi ya mji wa mimba na mirija ya uzazi (PID)
  • Endometriosis
  • Saratani ya mji wa kizazi; kwa kinamama waliofikia umri wa ukomo wa hedhi. Wakianza kupata hedhi isiyokoma huweza kuwa dalili ya ya saratani ya mji wa kizazi

ATHARI ZA HEDHI NZITO KUPITA KIASI KWENYE AFYA

  • Hedhi nzito kupita kiasi huchangia wanawake wengi kupata upungufu wa damu
  • Hedhi kuwa nzito kupita kiasi huweza kuwa ni dalili ambao unahitaji tiba ya haraka
  • Huweza kuchangia kudhoofisha afya ya akili ya mwanamke ikiwemo kujiamini na wasiwasi

Nini hufanyika unapomuona daktari kuhusu tatizo la kupata hedhi kupita kiasi ?

  • Unapomuona daktari atachukua historia ya afya yako kwa ujumla
  • Historia ya afya ya uzazi na mzunguko wako wa hedhi
  • Historia ya dawa zote unazotumia
  • Daktari atahitaji kukufanyia vipimo vya mwili ili kuangalia kama kuna kisababishi kinachochangia hedhi kutoka kwa wingi
  • Daktari naweza chukua damu kupima wingi wako wa damu , kiwango chako cha homoni za uzazi pia na vipimo vingine kulingana na alivyokuona
  • Datari anaweza kukufanyia ultrasound ili kungalia mji wa uzazi na via nyingine za uzazi kama kuna tatizo

Je ni tiba aina gani hutumika kutibu tatizo la kupata hedhi nyingi kupita kiasi?

Tatizo la kupata hedhi nyingi kupita kiasi hutibiwa kulingana na chanzo kilichosababisha tatizo hilo, afya yako kwa ujumla na uchaguzi wako tiba; baadhi ya tiba ni pamoja na :

  • Tiba ya dawa zenye homoni
  • Tiba za dawa za kugandisha damu — Hutolewa iwapo hedhi inayotoka ni nyingi sana
  • Upasuaji wa kuondoa vivimbe vya fibroids
  • Tiba ya kukwangua kuta za mji wa mimba
  • Tiba ya kuziba mishipa ya damu ya mji wa kizazi. Huitwa “uterine artery embolization”

Imeandaliwa na Dr Norman Jonas


KWA MATATIZO HAYA YOTE YA HEDHI CHECK INBOX 0758286584 UPATE MSAADA,TUMA UJUMBE UTAJIBIWA KWA HARAKA ZAIDI.

TATIZO LA KUKOSA HEDHI

➡️ Ombeni Mkumbwa

Wanawake wengi sana siku hizi wanasumbuliwa na tatizo hili la kukaaa mda mrefu bila kupata Hedhi ya mwezi.

Wengine wanaweza kukaa miezi miwili,sita au hata mwaka bila kupata hedhi kabisa.

ZIPO SABABU MBALI MBALI ZINAZOCHANGIA TATIZO HILI IKIWEMO; 

✓Matumizi ya baadhi ya njia za Uzazi wa mpango kama Sindano n.k

✓Mimba au ujauzito huweza kukata hedhi ya mwezi

✓Lakini pia swala la magonjwa au infection kitaalam, Mfano kama PID, n.k

✓Swala la kuvurugika kwa vichocheo vya mwilini kitaalam hujilikana kama "HORMONE IMBALANCE" hili nalo huweza kuchangia kwa kiasi kikubwa mwanamke kukosa hedhi ya mwezi.


KUMBUKA; MATIBABU YA TATIZO HILI YANATEGEMEA NA CHANZO CHA TATIZO,KWAHYO NI VIZURI KUONGEA KWANZA NA MTAALAM WA AFYA ILI KUJUA CHANZO CHA TATIZO LAKO KABLA HATA YA KUANZA MATIBABU

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!