Matibabu ya mba wa kichwani
Mba unaweza kupotea ghafla bila matibabu au unaweza kuhitaji kutunza kichwa na nywele kwa kutumia shampoo iliyo na dawa. Mara nyingine mba katika kichwa unaweza kuchukua wiki nyingi kutibika. Baadhi ya matibabu ya mba wa kichwani yanaweza kuwa ya tiba asili au tiba ya kisasa. Inashauriwa zaidi kutumia tiba ya asili kutibu mba wa kichwani, mojawapo ya tiba hizo za asili ni kama:
Matumizi ya mafuta yakupika nyumbani,mafuta ya nazi na juisi ya kutengeneza ya alovera. Juisi ya alovera inaweza kutumika kama shampoo ya kuosha kichwa na nywele na mafuta ya nazi kwaajili ya kulainisha ngozi na nywele.
Matumizi ya juisi ya limao, juisi ya limao ina asidi ya citric inayoweza kushambulia fangasi zinazosababisha ukurutu wa ngozi ya kichwa na pia inasaidia kupandisha juu ngozi zilizokufa juu na kuweza kuzisafisha kwa urahisi. Kamua limao na upate juisi ambayo itatumika kusugua kichwani kisha suuza na maji,fanya hivi kila ukitaka kuosha nywele.
Utajikinga vipi usipate mba wa kichwani
Ni vema kchukua hatua ili kuzuia mba kichwani ili usifikie hatua ya hatari zaidi, yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayoweza kufuatwa ili kupunguza au kutokomeza kabisa mba kichwani:
Kula kawaida, mlo wenye afya ulio jumuisha matunda na mbogamboga kwa wingi. Punguza vyakula vyenye mafuta, sukari na chumvi kwa wingi.
Safisha kichwa na nywele zako walau mara tatu mpaka nne kwa wiki, na suuza kwa maji mengi.
#afyadarasa
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!