MAUMIVU MAKALI YA KICHWA
. Kipandauso (Migrain)
Aina hii ya maumivu ya kichwa ya awali ndiyo iliyoenea sana na watu wengi wanaosumbuliwa na maumivu ya kichwa ya mara kwa mara huwa na tatizo hili. Maumivu haya yanaweza kuwa ya upande mmoja; lakini yanaweza kuwa katika paji la uso pia na kusikika katika eneo lote la paji la uso, na shingo.
Aina hii ya maumivu ya kichwa huwa ni ya “kichwa kugonga” (throbbing pain) na huambatana na dalili kama vile kichefuchefu na/au kutapika, kizunguzungu, macho kushindwa kuona vizuri, macho kuuma yanapoangalia mwanga. Aina hii ya maumivu ya kichwa huzidishwa na kutembea au kujisogeza kwa namna yoyote, na mgonjwa hujisikia nafuu akipumzika/kulala; kwa kawaida, maumivu haya huwa makali kwa muda wa masaa 1-2, na yanaweza kuchukua kati ya saa 4 hadi 72. Vitu ambavyo huweza kusababisha mtu mwenye tatizo la migraine kuanza kuumwa kichwa (triggers) ni kama vile vinywaji vyenye kemikali ya caffeine au pombe/sigara, mawazo, uchovu/usingizi, hasira, kwa kinadada kama akiwa anakaribia siku zake, au kwenye siku zake, mwanga mkali/sauti.
Aina hii ya maumivu ya kichwa pia huwasumbua zaidi wanawake ambao wako katika umri wa kuweza kushika mimba ambao ndio wameanza kupata hedhi zao kipindi cha karibuni. Pia, migraine huweza kurithiwa kutoka kwa wazazi kwa sababu mara nyingine husababishwa na vitu ambavyo viko kwenye vinasaba (genetics) za uzao husika.
Pia, aina hii ya maumivu ya kichwa mara nyingi hutanguliwa na ‘dalili za kabla’ (aura), ambazo hutokea kwa kati ya dakika 5-20, na hudumu si zaidi ya dakika 60; dalili hizi za kabla zinaweza kuwa kizunguzungu, kichefuchefu,mwili kukosa nguvu, n.k.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!