Maumivu ya korodani ni tatizo linalosumbua sana wanaume,mara nyingi husababishwa na maambukizi ya bakteria au magonjwa ya zinaa,kutokunywa maji mengi,misuguano inayoathiri moja kwa moja ngozi na mirija ya ndani ya korodani hizi ambayo inaweza kusababishwa na uvaaji wa nguo za ndani zinazobana sana,kujiviringisha kwa mirija ya mbegu za kiume,kujikusanya kwa maji na uchafu,ngiri,saratani ya korodani au hata sababu ya kupatwa na ajali
Kama unasumbuliwa na maumivu haya kwa siku kadhaa jitahidi unywe maji mengi sana na usitunze mkojo.Wakati huo asubuhi,mchana na jioni hakikisha unapangusa eneo la korodani zako kwa dakika 5 kwa kutumia maji ya barafu au hata barafu yenyewe.Kwa wasio na uwezo wa kupata mabonge ya barafu chemsha maji yawe vuguvugu kisha weka chumvi kidogo,jikande taratibu kwa dakika 5 tu pia asubuhi,mchana na jioni.Zikipita siku 3 baada ya kufanya hivi na maumivu bado yanakusumbua basi fika hospitalini haraka ili uchunguzwe na kusaidiwa
WANAUME TUMEELEWANA?
#afyadarasa #afyacheck_
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!