MICHIRIZI YA NGOZI HUSABABISHWA NA NINI?(STRETCH MARKS)

🔻MICHIRIZI YA NGOZI HUSABABISHWA NA NINI?(STRETCH MARKS)

Michirizi ya ngozi(stretch marks/striae) mara nyingi hutokea tumboni, juu ya matiti, mapajani, kwenye makalio na kwenye hips. Michirizi huwa ni kawaida kwa wanawake wajawazito, haswa katika miezi 3 ya mwisho ya ujauzito. Matibabu huweza kufifiza michirizi lakini sio kuiondoa kabisa


INA MADHARA YOYOTE?

Michirizi haisababishi maumivu na wala haina athari nyingine yoyote ILA TU baadhi ya wanawake hawapendezewi na muonekano wa maeneo yao ya mwili yenye michirizi .

.

HUSABABISHWA NA NINI?

Michirizi husababishwa na kuvutika kwa ngozi ya mwili. Uwingi wa michirizi hutokana na mambo mbalimbali ikiwemo hali za kurithi, mvutano wa ngozi na Homoni ya Cortisone. Hormone ya cortisone huhusika kufifisha nyuzinyuzi zinazoleta mvutano katika ngozi (elastic fibers)


VIHATARISHI 

1. Kuwa Mwanamke

2. Historia katika familia/kurithi

3. Ujamzito (haswa kwa wajawazito wenye umri mdogo/mimba ya kwanza)

4. Unene 

5. Kuongezeka/kupungua uzito kwa haraka 

6. Kutumia sana madawa ya jamii ya corticosteroids kama vile, prednisone

7. Upasuaji wa kuongeza makalio, matiti ama hips


NINI CHA KUFANYA KUIONDOA?

Kama unaona michirizi inakunyima raha unaweza kupaka mafuta katika maeneo yenye michirizi mara moja kwa siku. Mchanganyiko huo uwe na;

1. ½ kikombe cha mafuta ya zaituni (olive oil)

2. ½ kikombe cha ute wa aloe vera

3. Capsules 6 za vitamin E na Capsules 4 za Vitamin A. Pasua capsules hizo ungaunga wake uchanganye pamoja na olive oil na aloevera kisha upake. Kama utatengeneza mchanganyiko zaidi unaweza Kutunza katika jokofu. Mchanganyiko huu ni salama tofauti na cream nyingi zinazouzwa ambazo hazijathibitishwa na mamlaka husika

Cc:afyabongo #afyaclass

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!