MWANAMKE KUSHINDWA KUBEBA MIMBA

  SABABU ZA MWANAMKE KUSHINDWA KUPATA MIMBA 

➡️ Ombeni Mkumbwa

Utangulizi

Kumekuwa na wimbi kubwa la Wanawake wanatafta watoto au kubeba mimba bila mafanikio,Soma makala hii ujifunze na kuongeza maarifa Juu ya tatizo hili.

SABABU ZA MWANAMKE KUSHINDWA KUBEBA MIMBA

Zipo sababu nyingi sana ambazo huchangia tatizo hili.Na siku hizi tatizo hili limekuwa kubwa mno, wanawake wengi wanatafta watoto bila mafanikio.

Sasa leo nmekuletea baadhi ya sababu ambazo huchangia mwanamke kutokupata Mimba au Ujauzito.

(1)Mirija ya Uzazi kuziba

(2)Uvimbe kwenye kizazi

(3)Mvurugiko wa vichocheo mwilini au kitaalam hujulikana kama Hormone Imbalance

(4)Magonjwa kama PID,FANGASI NA UTI.Wanawake wengi hawajui kama ukiwa na magonjwa kama haya yanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kwa mwanamke kutokupata mimba

(5) Pia mwanamke kutokushiriki tendo la ndoa siku za Hatari.Hii inachangiwa na wanawake wengi kutojua siku za Hatari katika mzunguko wao wa Hedhi.Hivo hubahatisha tu.

TATIZO LA LOW SPERM COUNT

➡️ Ombeni Mkumbwa


Low Sperm count- Ni tatizo linalohusisha kuzalishwa kwa kiwango kidogo cha mbegu za Kiume. Fahamu kwamba kiwango kikubwa cha Mbegu za kiume hufa njiani kabla ya kulikuta yai la mwanamke na kulirutubisha.

Kwahyo basi kama kiwango kikubwa cha Mbegu za mwanaume hufa njiani kabla ya kulikuta yai la mwanamke na kulirutubisha,ni dhahiri kwamba ukizalisha kiwango kidogo cha mbegu(low sperm count) basi hata uwezekano wa kumpa mwanamke mimba utakuwa mdogo.

Swala la kupata Ujauzito limekuwa likihusishwa na matatizo kwa wanawake tu.Lakini fahamu kuwa mwanaume anaweza kuwa chanzo cha Mwanamke kutokupata mimba akiwa na matatizo kama hili la LOW SPERM COUNT.

MATIBABU

Hali hii au tatizo hili linatibika kwa baadhi ya vyakula,na dawa pia za kutumia ili kurudhisha uwezo wa kuzalishwa kwa mbegu kiwango kinachohitajika.
Muone daktari au mtaalam wa afya kwa ajili ya msaada zaidi

🔺SUMMARY

Katika makala hii tumezungumzia mambo yafuatayo;

- Utangulizi wa makala au Introduction kwa kingereza
-  Sababu za wanawake wengi kushindwa kubeba mimba
- Matibabu ya tatizo hili
-Maelekezo ya kupata ushauri,elimu au Tiba kwa tatizo lolote la kiafya.


0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!