SABABU ZA MTOTO KULIA SANA WAKATI WOTE HASA HASA WAKATI WA USIKU
SABABU ZA MTOTO KULIA SANA WAKATI WOTE HASA HASA WAKATI WA USIKU
➡️ Ombeni Mkumbwa
Kwa nini watoto wanalia?
Unaweza kuwa na wasiwasi mkubwa na ikawa vigumu kutambua kwanini mtoto wako analia kila Mara. Mtoto mdogo hawezi kusema chochote,kwahyo basi,kupeleka ujumbe au mesegi yoyote kwa Mzazi kwa chochote kile,ni kupitia Kulia.
Watoto hulia kwa sababu nyingi, na kulia ndio njia kuu ya watoto kuwasiliana. Hii ndyo njia pekee ya kukuvuta wewe na kukufikirisha mawazo yako huku wakielezea mahitaji yao. Mara ya kwanza, inaweza kuwa ngumu kutafsiri kilio tofauti cha mtoto wako, lakini unapotumia muda mwingi kusikiliza, utakuwa bora kutambua na kukidhi mahitaji maalum ya mtoto wako.
Je wajua ukielewa aina tofauti za vilio kwa mtoto wako,unaweza kugundua mahitaji yake tofauti,Mfano akiwa na Njaa utagundua kilio cha Njaa,akiumwa pia utagundua kilio cha kuumwa.
🆑 HIZI HAPA NI BAADHI YA SABABU ZA MTOTO KULIA
- Kulia kutokana na kuhitaji Kulala au uchovu
- Tumbo likiwa linauma au kujaa gesi
- Mtoto akiwa na Njaa
- Kelele za Mazingira aliyopo mtoto huweza kumsababisha alie
- Shuhuli mbali mbali kama vile; wakati unambadilisha Nguo,unamsafisha n.k
- Mtoto akigundua kwamba kaachwa mwenyewe anaweza kulia sana
- Matatizo kama Colic, reflux n.k
- Mtoto akiwa na maumivu yoyote au akiwa mgonjwa lazima alie kupeleka Ujumbe kwamba kuna tatizo
- Mtoto kushituliwa kwa gafla,either na makelele ya mtu,au vitu kama mziki mkubwa n.k
- Mtoto kuingiwa na wasiwasi au hofu either kutokana na mazingira ya kigeni aliyowekwa,au baada ya kuhisi utofauti.
🔻Kumbuka;
Kuzuia mtoto wako asilie ni pale tu umegundua hitaji lake na kulitimiza. Kwahyo basi;
➖ Mpe chakula anachostahili kama akihitaji Chakula,Hapa nazungumzia vitu kama Maziwa n.k ili kutimiza haja yake
➖ Tibu magonjwa au maumivu yake,kama umegundua ana shida hyo
➖ Hakikisha hakuna vitu vinavyomletea kujaa Gesi tumboni kama Unyonyeshaji Usio sahihi ambao unahusisha mtoto kunyonya huku sehemu kubwa ya mdomo ipo wazi na haijazibwa vizuri na chuchu hivo mtoto kunyonya maziwa pamoja na Hewa
➖ Epuka kumstua mtoto kwa kelele zozote,ziwe zako,za mtu mwingine au mziki Mkubwa
➖ Hakikisha mtoto anapata mazingira rafiki ya yeye kulala,kila anapohitaji kulala
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!