SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

DALILI NA VIASHIRIA VYA KUWA NA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI.

SARATANI NI NINI?

Saratani ni hali ya ukuaji wa seli hai za mwili usio wakawaida au ulizidi kiwango,Kwahyo basi, Saratani ya shingo ya kizazi ni ukuaji usio wa kawaida wa seli hai zilizopo au zinazounda eneo la shingo ya kizazi.

Chanzo cha Saratani ya Shingo ya Kizazi

Saratani ya Kizazi au saratani ya shingo ya kizazi husababishwa na Kirusi aitwaye HUMAN PAPILLOMA VIRUS (HPV). kirusi huyu ndyo Mhusika mkuu wa Tatizo hili ambapo kitaalam tatizo hili la Saratani ya shingo ya Kizazi hujulikana kama "cervical Cancer"

KUNDI LILILOPO KATIKA HATARI YA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

➖ Watu wanaoanza kushiri tendo la Ndoa au mapenzi wakiwa na umri mdogo mfano kabla ya miaka 18 au 20.

➖ Watu wenye wapenzi wengi yaani Multiple parteners

➖ Wanawake wenye Umri mkubwa mfano miaka 50 na kwenda mbele

➖ Kuzaa katika umri mkubwa mfano miaka 48.

➖ wanaotumia dawa zozote zinazohusu kuongeza uzalishaji wa seli hai za Mwili.

🔺DALILI ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Saratani ya shingo ya kizazi katika hatua za awali haina dalili au viashiria vyovyote.

Kutokwa na damu katika tupu ya mwanamke (vagina) ambayo sio ya kawaida. Damu hii inaweza kuwa matone, au damu inayotoka katikati ya mzunguko wa hedhi (yaani baada ya hedhi kabla ya hedhi inayofuata) au damu itokayo kwa mwanamke ambae ameacha kupata hedhi.

Kutokwa na damu baada ya kujamiana baada ya tendo la ndoa.

Maumivu wakati wa kujamiana.

Dalili za saratani iliyosambaa ni kama zifuatavyo

Kutokwa na majimaji ukeni kusiko kawaida yenye harufu na maumivu ya tumbo chini ya kitovu.

Kupungua kwa hamu ya kula

Kupungua uzito

Kuhisi uchovu

Maumivu ya nyonga

Maumivu kwenye mgongo

Maumivu ya mguu

Mguu mmoja kuvimba

Kutokwa na damu nyingi kwenye tupu ya mwanamke

Kuvunjika mifupa (bone fractures)

Kutokwa na mkojo au kinyesi kwenye tupu ya mbele ya mwanamke.

MADHARA YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

(1) Kupoteza maisha kwa Mwanamke

(2) Kutolewa kizazi chote na kupoteza uwezo wa mwanamke kuzaa tena

(3) Kuvuja damu na kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa

(4) Kutokwa na harufu kama ya kitu kilichooza Ukeni

MATIBABU YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Endapo tatizo hili litakugundulika katika stage za mwanzoni kabsa,mwanamke atapata tiba na atapona kabsa.Lakini kama akachelewa na saratani hiii au kansa hii ikafika stage iv ni ngumu kupona.

Kwahyo basi kuna umuhimu sna wa Kujichunguka kila wakati na pale unapoona mabadiliko yoyote mwilin,wahi hosptal kwa ajili ya uchunguzi na matibabu

DALILI ZA MIRIJA YA UZAZI KUZIBA

➡️ Ombeni Mkumbwa

Tatizo la Kuziba kwa mirija ya uzazi huonyesha dalili zake mara chache sana. Wanawake wengi hushindwa kutambua kuwa wana tatizo la kuziba kwa mirija ya uzazi mpaka pale wanapokuwa wakijaribu kutafuta ujauzito lakini wasiupate. Hizi ni baadhi ya dalili zinazoweza kujitokeza kwa mwanamke mwenye tatizo la mirija ya Uzazi Kuziba;

(1)Maumivu makali wakati wa hedhi

(2)Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa

(3)Maumivu wakati wa kukojoa

(4)Kutokwa na uchafu ukeni,

(5)Mirija ya uzazi kuvimba na kujaa majimaji

(6)Maumivu makali chini ya kitovu

(7)Maumivu ya nyonga, nk.

JE USHAWAHI KUSIKIA TATIZO HILI? JIBU NDYO AU HAPA KWENYE COMMENT👇

#afyacheck_



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!