FANGASI UKENI VISABABISHI VYAKE,DALILI ZAKE,MADHARA YAKE NA TIBA YAKE
➡️ Ombeni Mkumbwa
Ugonjwa Wa Fangasi Ukeni au Sehemu Za Siri kwa kitaalam hujulikana kama
(Vaginal Thrush)
Summary: Fahamu kwanza Sehemu za Siri za mwanamke zilivyo pamoja na asili yake
Ndani ya Sehemu za Siri za mwanamke(UKE) Kuna bacteria wanaojulikana kama "Lactobacillus Bacteria" Na Fangasi ambao hawaleti madhara yoyote ambao wapo Katika Kiwango Kinacho Lingana au Balanced Mix.
Bacteria Hawa Na Fangasi Hizi Husaidia Sana Kuulinda Uke Na Maradhi Mbalimbali Endapo Uwiano Wake hautavurugika. Sasa basi hawa Lactobacillus Bakteria Hutoa Acid Ambazo Huzuia Fangasi Kukuwa Au Kuwa Wengi Zaidi.
Ugonjwa Wa Fangasi Za Ukeni Ni Ugonjwa Anaoupata Mwanamke Endapo Fangasi Watakuwa Wengi Zaidi Ya Bacteria Wazuri Waliopo Ukeni Au Kama Ph Ya Ukeni Imezidi Kiwango Cha Kawaida Kinachopaswa(Ph 3.5-4.5 Ndio Kiwango Kizuri Kiafya).
fangasi Za Ukeni Mara Nyingi Husababishwa Na Fangasi Waitwao Candida Albicans, Lakini Wakati Mwingine Ni Aina Nyingine Za Fangasi Na Hizi Ni Vigumu Sana Kutibika
HIZI NI BAADHI YA SABABU ZA KUPATA FANGASI UKENI
1.Mvurugiko wa vichocheo vya mwili au tatizo la Hormone Imbalance(Homoni Za mwili kuwa nyingi Sana Au Kushuka Sana.Hii Inaweza Kusababishwa Na; Ukomo Wa Hedhi,ujauzito,kuwa Katika Siku Za Mwezi au period, Matumizi Ya Dawa Za Kuongeza Kiwango Cha Hormon Za Kike n.k
2. Matumizi Ya dawa aina ya Antibiotics ambazo huuwa Bacteria Wazuri Na Kubadiri PH ya sehemu za Siri za mwanamke(UKE).
3.kufanya Mapenzi Na Mtu Aliye Na Ugonjwa Wa Fangasi Za Sehemu Za Siri Bila Kinga
4.kushuka Kwa Kinga Ya Mwili ambayo husababishwa Na Magonjwa Mbalimbali Kama Ukimwi, Kisukari, Upungufu Wa Madini,vitamini Na Virutubishi Mbalimbali Vya Mwili.
5. Kutokula mlo kamili au Balance diet kumbuka; ulaji Mbaya Hasa Kupendelea Vyakula Vyenye Sukari Kwa Wingi (Sukari Ni Chakula Kwa Fangas Hivyo Huongezeka).
6.kukosa Usingizi Na Msongo Wa Mawazo .
DALILI ZA UGONJWA FANGASI UKENI
Kwa mwanamke ambaye na Fangasi wa Ukeni huweza kupatwa na Dalili hizi zifuatazo;
(1)KUTOKWA NA UCHAFU UKENI
Kutokwa na Uchafu wenye Rangi Tofauti Mfano Maziwa,ambapo mara nyingi Hutokea katika Rangi hii.
(2)KUWASHWA SANA SEHEMU ZA SIRI
Pia asilimia kubwa ya Wagonjwa wa Fangasi Ukeni hupata sana miwasho sehemu za Siri
(3)KUOTA VIUPELE UKENI
Kuota viupele vidogo vidogo ukeni,Hii pia ni dalili ambayo hutokea kwa Wagonjwa wa Fangasi ukeni.
(4) KUPATWA NA VIDONDA AU MICHUBUKO SEHEMU ZA SIRI(UKENI)
Hii pia yaweza kuwa Mojawapo ya Dalili z Fangasi ukeni
(5) KUPATA MAUMIVU MAKALI WAKATI WA TENDO LA NDOA
Magonjwa mengi huweza kuleta tatizo hili kama Vile PID-maambukizi katika via vya Uzazi vya mwanamke,Uti,kuziba Mirija Ya uzazi,Uvimbe wa Kizazi na hata Fangasi pia kuweza kusababisha hali hii
(6) HALI YA NJE YA UKE KUVIMBA NA KUWA NYEKUNDU HASA KATIKA MDOMO NA MASHAVU YA NJE YA UKE
Dalili hii pia huweza kutokea kwa mtu mwenye Fangasi Ukeni ambapo huambatana na Hali ya kuwaka moto sehemu ya Ndani na Nje ya Uke
🔺MADHARA YA FANGASI UKENI
Fangasi ukeni huweza kusabibisha Madhara yafuatayo;
*Mwanamke kushindwa kubeba mimba hasa kwa fangasi Sugu
*Uke Mkavu na maumivu makali wakati wa Tendo la Ndoa
*Harufu mbaya ukeni
*Uchafu mwingi na wenye harufu mbaya kutoka ukeni
*Michubuko na kuwaka moto ukeni
TIBA YA FANGASI UKENI
➡️ Kama una dalili hizo au una tatizo hili la Fangasi ukeni ni vizuri kwenda Hospital au kukutana na wataalam wa afya kwa ajili ya kupata Dawa au Tiba sahihi kwako.
JINSI YA KUJIKINGA NA FANGASI WA UKENI
1.Epuka matumizi ya vitu vyenye kemikali katika kusafisha Uke Kama baadhi ya Sabuni
2. Epuka Tabia ya Kuvaa Nguo za ndani mbichi au ambazo hazijakauka,kwani hutengeneza mazingira mazuri kwa Ajili ya Fangasi hawa kuwepo.
3.Epuka Kutumia Marashi Yenye Chemikali Ukeni Na Kuingiza Vitu Mbàlimbali Ukeni Kama Vidole, Asali, Mgagani N.k
4.Epuka Kutawadha Kutokea Nyuma Kwenda Mbele Baada Ya Kujisaidia Haja Kubwa Au Ndogo
5.Hakikisha kama mpenzi wako ana ugonjwa huu wa fangasi,anapata tiba sahihi na anapona kabla ya kushiriki tendo la Ndoa au kufanya chochote kama kuwa pamoja au karibu n.k
6.Safisha Uke Na Kujifuta Kwa Kitambaa Safi Ilikuuacha Mkavu
7.Kuwa mwangalifu sana hasa kipindi cha Ujauzito au ukiwa unatumia dawa ambazo huweza kushusha kinga yako ya mwili
8.Vaa Chupi Zitengenezavyo Kwa Vitu Harisi Kama Pamba Na Hariri
9.Epuka Ulaji Mbaya Wa Chakula Hasa Punguza Vyakula Vyenye Kukupayia Sukari Kwa Wingi Mwilini
10.Tumia Pads Zisizo Na Kemikali Na Zenye Vitu Vya Kukulinda Na Maambukizi,kukufanya Uwe Mkavu Na Huru.
Kumbuka; CANDIDA ALBICANS
Hawa ndyo huleta fangasi ukeni kwa asilimia kubwa.
Kama unatatizo hili tuwasiliane inbox 0758286584 ukituma UJUMBE utahudumiwa kwa Haraka zaidi.
#afyacheck_
TATIZO LA KUTOKWA NA UCHAFU UKENI
➡️ Ombeni Mkumbwa
Kutokwa na Uchafu wenye Rangi Tofauti Mfano Maziwa,ambapo mara nyingi Huambatana na Miwasho sehemu za Siri.Hizi ni Dalili za Fangasi Ukeni.
Kama unatatizo hili tuwasiliane inbox 0758286584 ukituma UJUMBE utahudumiwa kwa Haraka zaidi.
afya
afyaclass
afyatips
magonjwa
magonjwa ya wanaume
magonjwa ya wanawake
magonjwa ya watoto
makala
mpya
muhimu
new
post
uzazi
videos
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!